- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: UPANUZI WA BANDARI YA DAR KUPAISHA UCHUMI WA TANZANIA
DAR ES SALAAM: Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk John Pombe Magufuli amesema upanuzi wa Bandari ya Dar es Salaam utachochea utachochea miradi mingine kama vile mradi wa Reli ya kisasa ya standard gauge.
"Ufanisi na utendaji mzuri wa reli ya standard gauge utategemea ufanisi wa bandari hii, hivyo mtaona ni jinsi gani ni muhimu. Upanuzi huu utaongeza shehena ya mizigo na hivyo kuwezesha serikali kukusanya mapato," amesema Rais Magufuli.
Amesema mradi huu Unatarajiwa kukamilika kwa miezi 36 kama mkataba unavyosema, lakini akasisitiza kuwa anataka miezi 30 iwe imekamilika ikiwezekana hata miezi 28. Na kuongeza “fedha zipo sasa wakae miezi 36 hapa wanafanya nini," amehoji Rais John Magufuli.
"Ilitakiwa hii bandari iwe imepanuliwa zamani, wafanyabiashara walikuwa wanalalamika bila kusema sababu, tulikuwa na eneo ambalo halitoshi labda ulete mitumbwi na viboti hivi.
Tulikuwa tunasema tuna bandari lakini kumbe upande mmoja ni bandari ba upande mwingine ni mwalo," Rais John Magufuli Rais amesema bandari hiyo Ikishakamilika itakuwa ni ya mfano kwa sababu zitakuwa meli nyingi zinakuja kwa wakati mmoja, kutakuwa hakuna ucheleweshaji labda kama TPA wacheleweshe kwa makusudi.
Ameonya kuwa watakaochelewesha watakiona “Hao watakaochelewesha ndio tutalala nao vizuri," amesema Rais John Magufuli. "Pakiwa na facility nzuri hapa tutakuwa tunapromote uchumi wa nchi zingine. Bahati nzuri sisi ni wanachama wa SADC na EAC... hivyo watu kama milioni 500 watanufaika na bandari hii," ameongeza Rais John Magufuli.
"Serikali ya wamu ya tano imedhamiria kuboresha miundombinu ya usafiri na kudhihirisha hilo, tunaendelea na upanuzi wa bandari mbalimbali, viwanja vya ndegena barabara," amesema Rais John Magufuli.
"Bandari mmeanza vizuri lakini nataka kwenye hizi ICDs, hizi ziliwekwa kwa ajili mizigo ikijaa hapa ndio ipelekwe kule sasa hivi itapelekwa hata kabla haijajaa na kuna kamchezo fulani...mizigo inasemwa ni transit lakini inauzwa humu humu, kuna kampuni fulani inafanya huo mchezo wa kukwepa kodi fuatilieni hilo," ameelekeza Rais John Magufuli
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA), Deusdedit Kakoko amesema upanuzi wa Bandari ya Dar es Salaam ni muhimu kwa maendeleo na ufanisi wa Tanzania ya Viwanda.
Kakoko ameyasema hayo katika hotuba yake ya ufunguzi kwa Rais Dk John Magufuli wakati wa hafla ya uzinduzi wa Upanuzi wa Bandari hiyo katika viwanja vya bandari jijini Dar es Salaam.
“Bandari ya Dar es Salaam inahudumia asilimia 90 ya mizigo yote ya ndani na nje. Ina uwezo wa kuhudumia tani milioni 18" Deusdedit Kakoko, Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA) "Mradi wa uboreshaji wa bandari unatokana na umuhimu wa bandari hii katika kujenga uchumi.
Mradi huu ulianzishwa 2009 baada ya serikali kugundua kuwa bandari hii ingekuwa na uwezo mdogo siku za usoni kama hakutafanywa marekebisho makubwa" Deusdedit Kakoko, Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA) Amesema bandari ya Dar es Salaam Itaongeza uwezo wa kuhudumia shehena hadi kufikia tani milionj 28 ifikapo mwaka 2028.
Ameongeza kuwa mradi huo utakapokamilika utapunguza changamoto nyingi tulizonazo kama nchi. Kwa upande wake Mwakilishi wa Benki ya Dunia Bella Bird amesema uimara na umadhubuti wa Bandari ya Dar es Salaam ni muhimu kwa ukuaji wa uchumi wa Tanzania na nchi jirani hasa katika ukanda wa maziwa makuu.
"Hii bandari ni muhimu kwa uchumi wa Tanzania na nchi jirani," Bella Bird, Mwakilishi wa Benki ya Dunia. Amesema mradi unawakilisha mwanzo wa mchakato wa taratibu wa kuinua uwezo wa bandari ya Dar es Salaam na kuimarisha wajibu wake kiuchumi katika ukanda huu wa Afrika Mashariki na Kati.
"Nikupongeze wewe na serikali, kwa kuwa jana jiji la Dar es Salaam limetangazwa kuwa mshindi wa 28 wa usafirishaji duniani, na hiyo ni kutokana na mradi wa mabasi ya mwendo wa haraka. Tanzania inakuwa ni nchi ya kwanza kupata tuzo hii barani Afrika," Bella Bird, Mwakilishi wa Benki ya Dunia
Kwa upande wa Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa amesema Serikali imenza kutekeleza miradi mbalimbali katika bandari zote ikiwemo ununuzi wa mitambo.
Mradi huu utagharimu dola Marekani milioni 480, ikiwa mchango mmoja utatoka kwa TPA na wahisani wengine, mradi huu utatekelezwa katika awamu mbili. "Awamu ya kwanza itachukha miezi 28.
Serikali kupitia TPA itendelea kuboresha bandari za maziwa makuu ili kuimarisha biashara," Profesa Makame Mbarawa, Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano "Maboresho ya bandari hii yanafarajiwa kuwa chachu ya maendeleo kwa nchi yetu na nchi jirani na kupitia maboresho haya tunatarajia kuvutia shehena kubwa ya mizigo kutoka nchi za jirani," Profesa Makame Mbarawa, Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano:
source: Habarileo