- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: UNUNUZI WA GARI LA CHADEMA LAMTIA MASHAKA CAG
Dodoma. Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), Profesa Mussa Assad amesema Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kimenunua gari mpya aina ya Nissan Patrol kwa Sh147.76milioni na kusajiliwa kwa jina la mwanachama badala ya jina la Bodi ya Wadhamini ya chama hicho.
Profesa Assad ameongea leo Aprili 10, 2019 jijini Dodoma katika mkutano wake na wanahabari wakati akieleza taarifa za ukaguzi wa ofisi yake unaoishia Juni 30, 2018. “Gari hilo linaonyesha kwenye taarifa za fedha kama mkopo kwa mwanachama huyo bila kuwa na makubaliano ya mkopo yaliyosainiwa na mwanachama na bodi ya wadhamini ya Chadema,” amesema Profesa Assad.
Wakati huo huo Chama cha Mapinduzi (CCM) kinadaiwa Sh3.74bilioni kwa kutowasilisha michango ya kila mwezi kwenda Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF) hadi kufikia Mei, 2018.
Aidha, ameeleza vyama saba kikiwemo CCM na Chadema vilivyofanya matumizi ya Sh777.91milioni bila kuwa na nyaraka toshelevu na kushindwa kuthibitisha iwapo malipo hayo yalikuwa halali na iwapo yalihusiana na shughuli za vyama hivyo.
Amesema CCM hakikuwasilisha fedha hizo NSSF na kuwa na deni hilo linalojumuisha adhabu ya Sh2.73bilioni iliyotokana na ucheleweshwaji wa uwasilishaji wa michango hiyo.