Home | Terms & Conditions | Help

November 26, 2024, 7:29 am

NEWS: UMOJA WA ULAYA WAPATA RAIS MWANAMKE KWA MARA YA KWANZA

Bunge la ulaya limemthibitisha Waziri wa Ulinzi wa Ujerumani Bi Ursula Von der Leyen kuwa rais mpya wa Halmashauri Kuu ya Umoja wa Ulaya Jumanne, usiku na kuwa mwanamke wa kwanza kushika wadhifa huo wa fahari zaidi katika umoja huo, kwa kura 323-327.

Uthibitishwaji huo ulihitaji wingi wa kura 374 na waziri huyo wa ulinzi wa Ujerumani anaendoka alipita kwa ziada ya kura tisa.

"Najihisi mwenye heshima na furaha," alisema katika majibu yake ya kwanza. "Kazi iliyoko mbele yangu inanifanya kuwa mnyenyekevu."

Aliteuliwa nwa wakuu wa mataifa na serikali za Umoja wa Ulaya kama sehemu ya uteuzi jumla, lakini alihitaji kuungwa mkono na wabunge.

Aliibuka kama mgombea wa mwisho na wabunge wengi walikuwa na hasira kwa sababu hakuna kati ya mgombea wao alichaguliwa kwa wadhifa huo. "Ujumbe wangu kwenu nyote: Tushirikiane kwa kujenga," alisema.

Kuidhinishwa kwake kulikuwa sehemu muhimu ya nyadhifa za juu ambazo wakuu wa Umoja wa Ulaya walikubaliana juu yake mapema mwezi huu.



Chini ya makubaliano hayo, kundi la waliberali la Renew Europe lilimpata waziri mkuu wa Ubelgiji Charles Michel kama rais wa Baraza la Ulaya na Wasoshalisti walipata nafasi ya juu katika bunge la Ulaya.



Chrsitine Lagarge kutoka Ufaransa alipendekezwa kuwa mkuu wa benki kuu ya Ulaya. Von der Leyen aliwamabia wabunge mjini Strasbourg Jumanne kuwa suala la jinsia litakuwa sehemu muhimu ya kazi yake.



"Nitahakisha usawa kamili wa kijinsia," katika timu yake ya makamishna 28.