- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: UMOJA WA ULAYA WALAANI SHAMBULIO LA TUNDU LISSU
Dar es salaam: Jumuiya ya umoja wa Ulaya (EU) umelaani tukio la kushambuliwa kwa kupigwa risasi Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Antiphas Mughwai Lissu.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa kwa vyombo vya habari leo (Septemba 9, 2017) jijini Dar es Salaam, umoja huo unaalani tukio hilo huku wakitoa mwito kwa mamlaka husika kuwachukulia hatua za kisheria wahusika.
“Jumuiya ya Umoja wa Ulaya nchini Tanzania inaungana na Serikali ya Tanzania, Bunge la Tanzania na mashirika ya kiraia kulaani vikali jaribio lililohatarisha maisha ya Tundu Antiphas Mughwai Lissu, Mbunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Jimbo la Singida Mashariki,” inaeleza taarifa hiyo ya EU.
Kwa mujibu wa taarifa hiyo, jumuiya ya Umoja wa Ulaya nchini Tanzania inaomba mamlaka husika kuwachukulia hatua za kisheria wale wote waliohusika na shambulizi hilo, walilolitafsiri kuwa ni “lisilofaa dhidi ya demokrasia.”
“Jumuiya ya Umoja wa Ulaya nchini Tanzania inaungana na Watanzania wote kuwapa moyo familia ya mbunge na kuzidi kumuombea apone haraka,” inahitimisha taarifa hiyo.
Tundu Lissu alishambuliwa kwa risasi Septemba 7, 2017, akiwa nyumbani kwake mjini Dodoma kwa ajili ya mapumziko baada ya kikao cha Bunge la Jamhuri ya Muugano wa Tanzania.
Mashambulizi dhidi yake yalihusisha ufyatuaji wa risasi hadi 32 na kati ya risasi hizo, ni tano ndizo zilizompata katika mguu, mkono na tumbo.
Kwa sasa anaendelea kupatiwa matibabu katika Hospitali ya Aga Khan jijini Nairobi, nchini Kenya.