Home | Terms & Conditions | Help

November 25, 2024, 10:37 am

NEWS: UMMY AWACHANA WAHUDUMU WA AFYA

DODOMA: WAZIRI wa afya , maendeleo ya jamii,jinsia , wazee na watoto UMMY ALLY MWALIMU Amewataka wahudumu wa afya kuacha kufanya kazi kwa mazoea na matokeo yake wafanye kazi kwa bidii ili kuokoa maisha ya ndungu zetu walioathirika na ugonjwa huu.

Waziri huyo ameyaeleza hayo wakati wa ufunguzi wa mkutano wa kwanza wa kupitia utekelezaji wa mkakati wa ubnoreshaji wa kasi ya uibuaji wa wagonjwa wa kifua kikuuu nchini katika ukumbi wa kilimani landmark mjini Dodoma Amesema changamoto iliyokuwepo hapa nchini ya kuwahudumia wagonjwa wenye kifua kukuuu ni utoweza kuifikia sehemu kuwa ya wagonjwa wa kifua kikuu kiasi cha wagonjwa zaidi ya laki 100,000 kwa kila mwaka.


UMMY amesema utekelezaji wa mkakati huu ulianza mnamo julai 2016 ambapo hospital ya rufaa ya mkoa wa Dodoma katika miezi 6 baada ya kuanza kutekelezaji wa mkakati huu wameongeza wastani wa kuibua wagonjwa wa kifua kikuu kutoka 28 hadi 54 kwa mwezi huku jumla ya vituo 187 mikoa 16, wilaya 48 nchini vimeweza kuanza utekelezaji wa mkakati huu kiwamo mikoa wa Mbeya na Dodoma