Home | Terms & Conditions | Help

November 24, 2024, 6:53 am

NEWS: UMMY ATILIA MKAZO KWENYE AFYA JUU YA UGOJWA WA MARALIA

Dodoma: Ikiwa leo ni maadhimisho ya siku ya ugonjwa wa maralia duniani serikali ya jamuhuri ya muungano wa Tanzania imesema kuwa imefanya juhudi kubwa katika kupambana na ugonjwa huo na tayari vyandarua vyenye viwatilifu vya muda mrefu zaidi ya milioni 27 vimekwisha gawiwa kwa jamii bila malipo

bila malipo ambapo pia ametoa onyo kwa wahudumu wa afya katika vituo vya umma

Imekiri kutokufanya vizuri katika mapambano ya kutokomeza ugonjwa huo ambapo takwimu zinaonyesha wastani wa watu milion 12 huugua ugonjwa wa maralia kila mwaka

Hayo yametabainishwa hii leo na waziri wa afya,maendeleo ya jamii,jinsia,wazee na watoto Mh.Ummy Ally Mwalimu alipokuwa akizungumza na viongozi wa wizara ya afya pamoja na waandishi wa habari ofisini kwake mkoani Dodoma Bila ambapo pia sambamba na hayo ametoa onyo kali kwa wahudumu wa afya katika vituo vya umma

Mh.mwalimu amesema serikali inatumia maadhimisho haya kuihamasisha jamii kuhusu umuhimu wa kutambua dalili za maralia mapema,kuwahi kituo cha kutolea huduma kwa ajili ya vipimo pamoja na kuhimiza matumizi sahihi ya dawa ya kutibu ugonjwa huo na kuelezea takwimu za ugonjwa huo

Lakini pia kumekuwepo na baadhi ya vituo vya afya vinavyotoa majibu ya uwepo wa ugonjwa wa malaria kwa mgonjwa ili hali si kweli kwa ajili ya kujipatia kipato,kutokana na suala hilo mh.ummy pamoja na kiongozi upande wa uchunguzi na matibabu wa maralia dr.sixbert mkude wanatoa tamko.

Ugonjwa wa maralia bado unatajwa kuwa ni ugonjwa hatari nchini na wakati serikali inajitahidi kupambana kuutokomeza ugonjwa huo wananchi wameshauriwa kuwa na matumizi sahihi ya vyandarua wanavyopatiwa,na kauli mbihu katika maadhimisho haya ni shiriki kutokomeza maralia kabisa kwa manufaa ya jamii