- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: UMMY AMSIMAMISHA KAZI MKURUGENZI WA MAABARI YA TAIFA
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu amemwelekeza Katibu Mkuu (Afya), kuwasimamisha kazi mara moja Mkurugenzi wa maabara hiyo, Dk. Nyambura Moremi na Meneja Udhibiti wa Ubora, Jacob Lusekelo ili kupisha uchunguzi.
Aidha Waziri Ummy ameunda kamati ya wataalamu wabobezi kwa ajili ya kufanya uchunguzi wa mwenendo wa Maabara ya Taifa ya Afya ikiwamo mfumo mzima wa ukusanyaji na upimaji wa sampuli za corona.
Waziri Ummy amechukua hatua hiyo ikiwa ni utekelezaji wa changamoto zilizobainishwa na Rais John Magufuli jana Jumapili Mei 3, wilayani Chato alipokuwa akimwapisha Waziri wa Katiba na Sheria, Mwigulu Nchemba, katika maabara hiyo.
Kamati hiyo ya watu 10, itaongozwa na Profesa Eligius Lyamuya kutoka Chuo Kikuu cha afya na Sayansi shirikishi Muhimbili (Muhas) tayari imeanza kazi na itatakiwa kuwasilisha ripoti yake kwa waziri kabla ya Mei 13, mwaka huu.