Home | Terms & Conditions | Help

November 27, 2024, 3:41 am

NEWS: ULINZI UMEKUWA MKALI KWENYE KESI YA FREEMAN MBOWE

Dar es Salaam: Mahakama ya Rufaa na Mahakama Kuu jijini Dar es Salaam Leo hali imekuwa tofauti kufuatia kuwepo kwa ulinzi mkali hali iliyosababisha kuwepo kwa taharuki makamani hapo kwa baadhi ya wananchi.

Kuna magari ya polisi likiwemo la maji ya kuwasha yakiwa yameegeshwa pembezoni mwa mahakama hizo huku polisi wenyewe silaha wakifanya doria za kutembea huku na kule kuimarisha ulinzi. Polisi imezuia watu kupita pembezoni mwa Mahakama ya Rufani badala yake imewataka wapite ng'ambo ya pili.

Muakilishi imeshuhudia baadhi ya watu kuzuiwa kupita eneo hilo na kuamriwa kupita sehemu nyingine. Pia kuna ukaguzi maalum katika lango la kuingilia Mahakama ya Rufani.

Ulinzi huo unatokana na kesi mbili tofauti kusikilizwa leo Jumatatu Februari 18, 2019 katika mahakama hizo kwa nyakati tofauti.

Katika Mahakama ya Rufaa, inatarajia kusikilizwa rufaa ya Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP) dhidi Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Freeman Mbowe na mhazini wa Baraza la Wanawake Chadema (Bawacha), Esther Matiko.

DPP alikata rufaa Mahakama ya Rufani kupinga uamuzi wa Mahakama Kuu, kukubali kuendelea na usikilizwaji wa rufaa ya wabunge hao ya kupinga uamuzi wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Dar es Salaam, Kisutu kuwafutia dhamana.