- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: UKOSEFU WA VYOO WAWA GUMZO KWA SERIKALI
DODOMA: MTANDAO wa elimu nchini umesema kutokana na utafiti waliofanya mwaka 2016 mpango wa elimu bila malipo umeongeza unadikishaji wa wanafunzi kwa asilimia 43 huku upungufu wa vyumba vya madarasa,vyoo na waalimu ukiongezeka ambapo kwa sasa mwalimu mmoja anafundisha wanafunzi zaidi ya 160 katika darasa moja.
Mwenyekiti wa bodi ya mtandao wa elimu nchini JOHN KALAGHE akizungumza mjini Dodoma wakati wa mkutano wa wadau wa elimu nchini na nje ya nchi amesema serikali inapaswa kuchukua hatua za haraka kutatua changamoto hizo ili wanafunzi hao wapate elimu yenye ubura.
Amesema kwa mujibu wa sera ya elimu nchini mwalimu mmoja anatakiwa kufundisha wanafunzi 45 katika darasa moja huku tundu moja la choo likitakiwa kutumika na wavulana 25 wasichana 20 ambapo kabla ya mpago wa elimu bila malipo mwalim mmoja alikua akifundisha wanafunzi 70.
Naye katibu mkuu wa wizara ya elimu sayansi na technologia dk Leonard Akwilapo wakati akifungua mkutano huo wenye lengo la kutathmini hali ya elimu nchini amesema kuwa serikali itaendelea kutekeleza malengo endelevu katika sekta ya elimu ili kuhakikikisha hakuna mtoto anayeachwa katika kupata elimu.
Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais TAMISEMI anayeshughulikia Elimu Tixon Nzunda amesema kuanzia sasa majengo yote ya shule yanayojengwa katika mfumo wa sasa hayatakuwa na ngazi ili kila mtoto aweze kuyafikia hususan watoto wenye ulemavu.