Home | Terms & Conditions | Help

November 25, 2024, 1:31 am

NEWS: UJUMBE WA HUSSEIN BASHE KWA RAIS MAGUFULI

Dodoma: Mbunge wa Nzega mjini Mh. Hussein Mohammed Bashe leo amempongeza Rais Magufuli kwa hatua ya kuonesha Uthubutu dhidi ya Hatua anazozichukua kama Rais juu ya Uboraji rasilimali, Bashe alisema kuwa hakuna jambo liliwahi kufanikiwa pasipo kuwepo Uthubutu, nakama kila mmoja atakuwa anakimbia kuthubutu, ni nani atakayeanza? na tuanze lini? alihoji Bashe alisem Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania John Pombe Magufuli amethubutu"


Pia Bashe aliomba kwa kamati za uchunguzi waende kwenye mgodi wa alimasi wa Williamson ambapo alisema kuna wizi mkubwa pale
"Lakini pia niombe kwa Kamati zinazoendelea na zitakazokuja zifanye pia uchunguzi kwenye mgodi wa Almasi wa Williamson ambapo kuna wizi mkubwa unaendelea unaofanywa na kampuni yenye kibali kwa kushirikiana na kampuni ya Ulinzi wa mgodi huo ambapo kampuni ya Ulinzi inaendeleza shughuli za Uchimbaji pembezoni mwa mgodi huo kinyume na sheria.

Mwisho nimuombe Mheshimiwa Rais aruhusu mikataba ya madini ijadiliwe upya ili wabunge kwa umoja wetu tuungane na Rais wetu katika kuboresha mikataba hii iweze kunufaisha taifa na kujenga mazingira bora ya usimamizi wa rasilimali zetu nchini.
Kujadiliwa kwa mikataba hii kutatoa fursa kwa watanzania wote chini ya Rais John Pombe Magufuli kusimama pamoja kama Taifa kulinda rasilimali zetu dhidi ya wawekezaji na watu wachache wenye nia ovu dhidi ya watanzania walio wengi.