Home | Terms & Conditions | Help

November 24, 2024, 9:11 am

NEWS: UJIO WA MAKAO MAKUU DODOMA WALETA NEEMA KWA MADEREVA BAJAJI.

Dodoma: Baadhi ya Wafanyabiashara ndogondogo wakiwemo madereva wa Bajaji katika Manispaa ya Dodoma wameeleza kunufaika na ujio wa Makao makuu huku wengine wakilalamikia kupanda kwa bei ya vitu hususani vyakula na hivyo biashara kuwa ngumu.

Hayo yameelezwa leo Mjini Dodoma na baadhi ya wafanyabiashara hao wakati walipokuwa wakizungumza na vyombo vya habari kuhusiana na fursa ya ujio wa makao makuu.

Kwa upande wao madereva wa Bajaji walionekana kufurahishwa na ujio huo nakusema kuwa kuwepo kwa ujio wa Makao makuu hivi sasa kumekuwepo na msongamano mkubwa wa watu pamoja na magari katika maeneo mbalimbali ya mji wa Dodoma ambavyo vimeelezwa ni moja ya sababu ya vitu kupanda bei.