- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: UJERUMANI YAFUNGA MIPAKA YAKE KUZIA KUENEA KWA CORONA
Serekali nchini Ujerumani imeamua kufunga mipaka yake na mataifa ya jirani ya Austria, Uswisi na Ufaransa kuanzia leo Jumatatu asubuhi katika hatua ya karibuni kabisa ya kupambana na kusambaa kwa virusi vya Corona.
Hayo ni kulingana na magazeti mawili ya Der Spiegel na Bild yaliyoripoti kuwa mamlaka za Ujerumani lakini zitaendelea kuwaruhusu wasafiri wanaovuka mipaka kila siku kwa ajili ya kwenda kazini pamoja na uingizaji wa bidhaa.
Hata hivyo hakuna taarifa juu ya iwapo Ujerumani inalenga kuifunga pia mipaka mingine ikiwemo kati yake na Poland, Uholanzi, Denmark na Jamhuri ya Czech. Hayo yanajiri wakati idadi jumla ya waliokufa kutokana na virusi vya corona duniani imepanda na kufikia watu 6,036.
Ongezeko hilo ni kutokana na vifo vipya 105 nchini Uhisapania moja ya taifa lililoathiriwa vibaya na virusi vya corona barani Ulaya.