- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
News: Ujenzi wa Hospitali za Wilaya na Vituo vya Afya washika kasi Nchini.
TANGA: Katika jambo mojawapo ambalo linaacha alama kubwa kwa utendaji bora unao wajali wananchi wanyonge hapa Nchini ni pamoja na zoezi kabambe linalo endelea la ujenzi wa hospitali 67 pamoja na uboreshaji wa Vituo vya Afya 350 chini ya Ofisi ya Rais TAMISEMI.
Kwasasa ujenzi huo unaendelea kwa kasi kubwa na kuleta furaha kubwa kwa wananchi wa maeneo mbalimbali hapa nchini. Hayo yamedhihirika katika Ziara ya Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI mkoani Tanga ambapo mkoa huo umeendelea kufanya vyema katika usimamizi wa miradi hiyo.
Waziri Jafo amehitimisha ziara hiyo ya Mkoani Tanga leo hii tarehe 31 January 2019 kwa kutembelea miradi hiyo kwa wilaya za Mkinga na Muheza na kuridhishwa na kasi ya ujenzi.
Aidha, Jafo amewataka viongozi wote katika Mikoa na Wilaya zote kukamilisha miradi hiyo ya ujenzi wa hospitali 67 kabla ya July Mosi 2019.