Home | Terms & Conditions | Help

November 26, 2024, 6:33 am

NEWS: UINGEREZA YAPATA WAZIRI MKUU MPYA BAADA YA KUSHINDA UCHAGUZI

Waziri wa zamani wa mambo ya kigeni wa Uingereza Boris Johnson amechaguliwa kuwa kiongozi wa chama tawala cha Conservatives nchini humo atakayechukua mara moja nafasi ya Bi Theresa May.

Großbritannien London | Boris Johnson wird neuer Premierminister (Reuters/T. Melville)

Hii inamaanisha Boris Johnson sasa atakuwa Waziri Mkuu mpya wa Uingereza baada ya May kutangaza kujiuzulu mwezi uliyopita.

Boris aliye na miaka 55 alimshinda mpinzani wake Jeremy Hunt kwa wingi wa kura katika uchaguzi wa wanachama wa chama cha conservatives hii leo.

Waziri huyo wa masuala ya kigeni wa zamani wa Uingereza ananatarajiwa kuchukua rasmi nafasi hiyo ya uwaziri Mkuu hapo kesho Jumatano (24.07.2019).

Ingelikuwa mshituko mkubwa iwapo uongozi huousingekwenda kwa Boris Johnson, meya wa zamani wa London ambaye amewavutia wanachama wa chama cha Conservative kwa kuahidi kufanikisha pale ambapo May alishindwa na kuiongoza Uingereza kujitoa kutoka Umoja wa Ulaya katika tarehe iliyopangwa Oktoba 31, kwa kupata makubaliano ama la.