- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: UHURU AWAKATAA MAAFISA WAPYA WA TUME YA UCHAGUZI
Dar es salaam: Chama cha Jubilee, cha rais wa sasa nchini Kenya Uhuru Kenyatta, kimepinga maafisa wapya tisa ambao ni wakuu wa Tume ya Uchaguzi nchini humo ambao wanatarajiwa kusimamia uchaguzi mpya mwezi ujao. Chama cha Jubilee kimewatuhumu maafisa wapya kwa kusema kuwa wanapendelea upande mmoja,
IEBC iliwateua maafisa 7 wakuja kusimamia uchaguzi unaokusudiwa kufanyika Tarehe 17 September mwaka huu, Maafisa hao wamechaguliwa baada ya kiongozi wa Upinzani nchini kenya Bw. Laila Odinga kuapa kutoshiriki kwenye uchaguzi kama maafisi wapya wa tume ya uchaguzi hawatateuliwa.
Maafisa hao ambao wanajumuisha mkuu wa kitengo cha Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (ICT) na msimamizi wa kituo cha taifa cha kujumlishia matokeo watahudumu kwa miezi mitatu.
Chama cha Jubilee kimesema: "Tuna habari za kuaminika kwamba kwenye orodha ya maafisa hao (watakaosimamia uchaguzi) kuna watu wanaofahamika wazi kuegemea upande Fulani."
"Ikizingatiwa makossa mengi ya kutotenda au ya kutenda ambayo yalichangia uchaguzi kufutiliwa mbali ambayo chanzo chake kilikuwa wafanyakazi wa IEBC, tunawasilisha pingamizi zetu kwa watu hawa tuliowataja hapa juu."
Muungano wa National Super Alliance (Nasa), ambao mgombea wake alikuwa waziri mkuu wa zamani Raila Odinga, ulikuwa umeitisha mabadiliko makubwa kwenye IEBC kabla ya uchaguzi mpya kufanyika.