Home | Terms & Conditions | Help

November 26, 2024, 11:55 am

NEWS: UHAMIAJI ZANZIBAR WASEMA WALIPEWA MAAGIZO KUMZUI ZITTO KUSAFIRI

Zanzibar: Mamlaka za Uhamiaji visiwani Zanzibar wamesema walimzui kusafiri nje ya nchi Kiongozi mkuu na Mbunge wa ACT- Wazalendo Zitto Zuberi Kabwe kunatokana na agizo walilopewa na Serikali ya Tanzania Bara ya Kuto safiri njee ya nchi.

Msemaji mkuu Uhamiaji Zanzibar, Sharif Bakar Sharif amenukuliwa na Gazeti la Mwananchi leo Jumatano Juni 12, 2019 akisema kuwa kilichofanywa na Uhamiaji ni kutekeleza agizo Serikali la kumzuia baada ya kuonekana kuna haja ya kuzuiwa kwa mujibu wa taratibu ya vyombo vya ulinzi na usalama juu ya utekelezaji wa maagizo ya Serikali.

"Sisi kwa kuwa ni sehemu ya vyombo vya ulinzi na usalama tulitekeleza agizo hilo la kutomruhusu kusafiri nje ya Tanzania na tayari tumeshamfikisha katika vyombo vingine vya sheria kwa ajili ya hatua zaidi za kisheria na kikanuni," amesema Sharif.

Zitto alikamatwa Jana Jumanne majira ya saa nane mchana, katika uwanja wa ndege Zanzibar wakati akiwa katika taratibu za kutaka kusafiri kwenda nchini Kenya baada ya kutoka kwenye kikao cha Chama chao.

Baadae baada ya kuachiliwa na Jeshi la Polisi Zitto alitoa taarifa ya kushikiliwa kwake kuwa inatokana na mashtaka yatokanayo na sheria ya Huduma za Habari 50(1)(a)

"Nimekamatwa tangu saa nane mchana Leo. Nimezuiwa na maafisa Uhamiaji kuwa sina ruhusa kutoka nje ya nchi. Sasa nipo Polisi kwa maelekezo ya TAKUKURU kuwa Nina mashtaka yatokanayo na sheria ya Huduma za Habari 50(1)(a)" alisema Zitto Kupitia Ukurasa wake wa twitter