- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: UHAKIKI WA VYETI WATISHIA AFYA ZA WAGONJWA HOSPITALI YA MPANDA
Dodoma: KUTOKANA na zoezi la uhakika wav yeti feki kwa sasa zoezi hilo limeanza kutishia afya za watu hususani katika vituo vya afya na hospitali jambo ambalo linaweza kusababisha wagonjwa kupoteza maisha kutokana na kukosa huduma.
Hayo yalijitokeza jana bungeni wakati Mbunge wa Viti Maalum, Rhoda Kunchela (Chadema) ambaye alilazimika kuomba mwongozo bungeni kwa kulitaka bunge lisitishe shughuli za bunge kwa lengo la kujadili jambo ambalo linaendelea katika hospitali ya Mpanda Manispaa.
Mbunge huyo aliomba mwongozo wa spika kwa kanuni za bunge 47(1) akisema kutokana na kuwepo kwa uhakiki wav yeti kwawatumishi wa Umma kwa sasa wagonjwa hawapati huduma katika hospitali ya Wilaya ya Mapanda Manispaa.
“Kutokana na uhakiki wa vyeti unaoendelea kwa sasa zaidi ya wagonjwa 20 ambao walitakiwa kutibiwa wamekosa matibabu jana (Juzi) siku nzima jambo ambalo wagonjwa hao wanaweza kupoteza maisha.
“Kutokana na tatizo hilo nanaomba wabunge waniunge mkono ili shughuli za bunge ziweze kuahirishwa ili kuweza kujadili jambo hilo ambalo kimsingi ni adha kwa wagonjwa hao” aliwasilisha Kunchela.
Kunchela aliomba mwongozo huo jana bungeni muda mfupi baada ya kumalizika kwa kipindi cha maswali na majibu ambapo wabunze zaidi ya sita waliomba miongozi kutokana na majanga mbalimbali ambayo yanaendelea kujitokea hapa nchini.
Kunchela pia alisema hospitali hiyo ambayo hutoa huduma kwa wagonjwa wengi alisema kama suala hilo halitatafutiwa ufumbuzi haraka wagonjwa wengi wanaweza kupoteza maisha kutokana na kukosa huduma za matibabu.
miongozo ya Kunchela unaangukia katika kanuni ya 47(1) ambayo inasomwa pamoja na kanuni ya 48.
“Lakini kanuni ya 47(4) inampa Spika mamlaka aridhike kama ombi hilo anaona jambo hilo kweli linahitaji kusitisha shughuli zilizombele yetu ili kujadili hoja hizo za dharura,”alisema.
Hata hivyo, alisema kwa hali anayoiona haoni kama suala hilo linahitaji kujadiliwa sasa.