Home | Terms & Conditions | Help

November 25, 2024, 3:32 am

NEWS: UHABA WA MITI KIKWANZO KWA WAFANYABIASHARA YA HEWA CHAFU TANZANIA.

MPWAPWA: Uhaba wa misitu katika baadhi ya maeneo nchini kumetajwa kuwa ni sababu ya Tanzania kukosa mamilioni ya fedha zinazotolewa na Makampuni Makubwa duniani yanayozalisha hewa chafu za viwandani.


Hayo yamebainishwa leo na Mkurugenzi wa Miradi wa Shirika la LEAD FOUNDATION Njamasi Chiwanga wakati wa kikao cha pamoja na Viongozi wa Vijiji wakiwemo Watendaji na Wengeviti katika Tarafa ya Mima na Kibakwe, Wilayani Mpwapwa ,Mkoani Dodoma.


Amesema kwa mujibu wa sheria za kimataifa za uhifadhi wa mazingira zinayataka makampuni makubwa yenye viwanda duniani kutoa sehemu ya faida kufadhili miradi ya mazingira.


Amesema kutokana hali hiyo shirika la Lead Foundation imeteuwa wakulima 18 kutoka katika kila kijiji katika tarafa hizo za Kibakwe na Mima kwa ajili ya kustawisha miti laki mbili kupitia njia ya kisiki hai.

Amesema hadi kufikia sasa shirika hilo kwa kushirikiana na vikundi hivyo 18 vya wakulima wa mfano wamefanikiwa kupanda jumla ya miti milioni 3.5.


Waziri wa Elimu Mstaafu katika serikali ya awamu ya kwanza chini ya Hayati Julius Nyerere na Askofu Mstaafu wa kanisa la kiinjili la kiluthel (KKKT)Dk. Simon Chiwanga, amesema uharibifu wa misitu katika Nchi hii ni mkubwa hivyo ameitaka jamii kutuza miti ili kukomboa ardhi iliyochakaa huku akidai misitu ni rasilimali muhimu hususani katika ulimwengu wa sasa ambapo kumekuwa na biashara ya uuzaji wa hewa chafu (Cabon Trade).


Kwa upande wake mmoja wa wakulima walio katika kikundi cha wakulima wa mmfano, Harold Madihi, amewataka viongozi wa Vijijini kusimamia mradi huo ipasavyo ili kuja kupata manufaa siku za mbeleni.