Home | Terms & Conditions | Help

November 25, 2024, 5:43 pm

NEWS: UGANDA IMEPIGA MARUFU WANANCHI KUVAA KOFIA KAMA ZA BOBI WINE

Serekali nchini Uganda imewazuia raia wa taifa hilo kuvaa kofia nyekundu ambazo zimekuwa kama alama ya wafuasi wa mwanasiasa kijana Robert kyagulanyi maarufu Bobi Wine na vuguvugu lake la "nguvu ya umma", ambalo anaamini litamuondoa madarakani rais Yoweri Museveni.

Tokeo la picha la Bobi Wine

Kofia hizo ambazo pia huvaliwa na baadhi wa wanajeshi wa Uganda, zilijumuishwa kwenye tangazo la kwanza kabisa kutolewa na serikali ya Uganda kuhusu mavazi ya wanajeshi na kuzitaja kama mali za serikali ambazo raia hawaruhusiwi kuzivaa.

Bobi Wine ameikosoa hatua hiyo, akisema ni kisingizio tu, lakini akisisitiza kwamba halitakuwa na athari yoyote.

Mwanamuziki huyo wa zamani, amekwishatangaza kugombea urais kwenye uchaguzi wa mwaka 2021, katika kinyang'anyiro kitakachamkutanisha na rais Museveni aliyehudumu tangu mwaka 1986.