- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: UFARASA WAFANYA MKUTANO WA KUMALIZA UGONJWA WA KIPINDUPINDU
Ni mara ya kwanza serikali, shirika la afya duniani, mashirika ya misaada na wafadhili wametoa ahadi kama hiyo.
Hii inakuja wakati Yemen inandelea kupambana na moja ya milipuko mibaya zaidi ya ugonjwa wa kipindupindu katika historia yake.
Ugonjwa wa Kipindu pindu katika karne ya 21 umeelezewa kama ''aibu kubwa kwa dunia,"
Ugonjwa huo ulitokomezwa nchini Uingereza na Marekani zaidi ya miaka 100 iliyopita , lakini unaendelea kusababisha vifo katika mataifa mengi yanayoendelea.
Si ghali kutibu ugonjwa huo na unaweza kuepukika kabisa ikiwa watu watapata maji safi na vyoo visafi
Lengo kuu katika mkutano wa leo litakuwa ni maeneo yanayoathiriwa zaidi na kipindupindu barani Afrika na Asia, ambako milipuko hutokea mara kwa mara.
Maafisa hao wataahidi pia kumaliza milipuko inayowakumba watu wengi inayosababishwa na mizozo au majanga ya asili.