Home | Terms & Conditions | Help

November 24, 2024, 7:06 am

NEWS: UCHAGUZI WA UFARANCE WAPAMBA MOTO WASHIDI WA DURU YA KWANZA

PARIS: Katika mchakato unao endelea nchini ufaransa wa kumsaka mshidi nwa kiti cha urais nchini humo ambapo Mgombea wa siasa za mrengo wa kati Emmanuel Macron na mgombea wa chama cha siasa kali za mrengo wa kulia Marine Le Pen wameingia katika duru ya pili ya uchaguzi wa urais nchini Ufaransa


Matokeo ya kura yamekuwa, Macron amejipatia asilimia 23.9 ya kura na Le Pen amepata asilimia 21.4. Kura za maoni zilizochapishwa hapo jana zinaonyesha kwamba Macron atamshinda Le Pen kwa urahisi katika duru ya pili.

Akihutubia baada ya ushindi wake hapo jana Macron alisema. Macron alisema tangu kuundwa kwa Jumuiya yake ya kisiasa mwaka mmoja uliopita, siasa za Ufaransa zimebadilika. Kiongozi huyo amesema anataka kuwa rais atakae wawezesha watu wanaotaka kuwa wabunifu na wenye ari ya kutenda kazi ili kuyafikia malengo yao kwa urahisi na haraka zaidi.


Mgombea mwingine aliyefanikiwa kuingia katika raundi ya pili ya uchaguzi kiongozi wa chama cha mrengo mkali wa kulia Marine Le Pen amewataka Wafaransa waitumie fursa ya kihistoria iliyopo.