- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: UCHAFU WASABABISHA 75% YA MAGONJWA KWENYE JAMII.
DODOMA: Zaidi ya asilimia 75 mpaka 80 ya magonjwa yanayowazunguka watu katika jamii yanatokana na uchafu.
Hayo yameelezwa na Mkuu wa Idara ya Mazingira na udhibiti wa taka ngumu wa Jiji la Dodoma,Dickson Kimaro katika wiki ya maadhimisho uzinduzi wa sera ya taifa ya Mazingira inayoendelea ambapo mkuu huyo wa Idara amesema zoezi zima la usafi linaloendelea litasaidia wananchi kujikinga na kuepukana na Magonjwa yataokanayo na uchafu.
Amesema suala la usafi na utunzaji wa mazingira ni suala la tabia na linatakiwa lianze katika jamii kwa kubadilika ndani na nje mazingira yawe nadhifu ambapo amewataka wananchi kila mmoja kufanya usafi kwenye kaya yake .
"Dodoma ni makao makuu ya nchi hivyo kama jiji la Dodoma tunatakiwa tuwe jiji la mfano kwakuwa ni Makao Makuu ya nchi yetu tuhakikishe jiji linakuwa safi
Na kuongeza kusema"Hii ni chachu tu katika kuhakikisha kila mmoja kwenye eneo lake ndani ya kaya ahakikishe anafanya lakini pia hapa Dodoma tumekuwa na kauli mbiu ya usafi wangu mita tano kwamba kila mmoja katika eneo lake hakikisha panakuwa pasafi," Amesema
Hata hivyo katika siku ya leo Februari 8 2022 wamefanya usafi katika eneo la Martin Luthar kuelekea Ilazo kwa kusafisha mitaro na kufyeka nyasi ambapo wananchi,viongozi na wanafunzi walijitokeza na kufanya zoezi hilo la usafi.
Nao wanafaunzi walioshiliki katika zoezi hilo wamesema usafi wa mazingira ni muhimu kwani huwasaidia kujikinga na magonjwa lakini pia wanavosafisha mazingira wanaondoa wadudu hatari kama nyoka na Nge hasa katika kipindi hiki cha mvua zinazoendelea kwani majani na nyasi yanaota kwa kasi.
Akiongea kwaniaba ya wenzake Salome Musisa mwanafunzi wa kidato cha Tatu shule ya sekondar Maria De Mattias amesema kuwa wamejipanga kujikita katika usafi ili waweze kufanya vizuri katika masomo yao.
"Tumejipanga kushilikiana na serikali sisi kama wanafunzi kuweza kufanya vizuri kwani Maendeleo ya kimazingira yanaweza kuendeleaza maendeleo ya kiuchumi na kufika mbali kama nchi au taifa,"Amesema wanafunzi Salome
Kwa upande wake Afisa Mtendaji wa Mtaa wa Nyumba 300 Kata ya Nzuguni Jemima Malau amesema kuwa zoezi la usafi mazingira limewahamasisha nawao kama watendaji wamekuwa wakiwahamasisha wananchi wao kufanya usafi .