- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: UBOVU WA GARI WAMZUIA HALIMA MDEE KUHUDHURIA KESI YAKE
Dar es Salaam. Mbunge wa Kawe (Chadema), Halima Mdee imeelezwa kuwa ameshindwa kufika katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu leo kusikiliza kesi inayomkabili ya kutoa lugha shafu dhidi ya Rais Magufuli baada ya gari lake kuharibika wakati akirejea jijini Dar es salaam akitokea Dodoma.
Maelezo hayo yametolewa mahakamani hapo leo Jumanne Oktoba 29, 2019 na Mdhamini wa Mbunge huyo Fareson Rukomo.
Mbunge huyo anakabiliwa na kesi ya kutoa lugha chafu dhidi ya Rais wa Tanzania, John Magufuli.
Wakili wa Serikali, Wankyo Simon amedai shauri hilo lilikuja kwa ajili ya usikilizwaji, kwamba shahidi waliyekuwa wakimtegemea hajafika mahakamani sambamba na mshtakiwa.
Baada ya maelezo hayo Hakimu Mkazi Mkuu, Thomas Simba alimtaka Rukomo kuieleza mahakama sababu za mbunge huyo kutofika mahakamani.
Mdhamini huyo alidai gari la Halima Mdee limeharibika kati ya Dodoma na Morogoro wakati akirudi jijini Dar es Salaam. "Nimepigiwa simu jana usiku wakati Mdee anakuja Dar es Salaam kwamba gari lake limeharibika kati ya Dodoma na Morogoro. Kanituma nije hapa kueleza,” amesema Rukomo. Baada ya maelezo hayo Hakimu Simba ameahirisha kesi hiyo hadi Novemba 8, 2019.
Katika kesi ya msingi inadaiwa Julai 3, 2017 katika ofisi za makao makuu ya Chadema zilizopo mtaa wa Ufipa wilayani Kinondoni, Mdee alitamka maneno dhidi ya Rais John Magufuli kuwa, ‘anaongea hovyo, anatakiwa afungwe breki,’ kitendo kinachodaiwa kuwa ni kumdhalilisha Rais na kusababisha uvunjifu wa amani.