- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: UBOHO KUPANDIKIZWA MWAKANI HOSPITALI YA BENJAMINI MKAPA.
DODOMA: Hospitali ya Benjamin Mkapa Kwa mara ya kwanza kwa kushirikiana na Afrika Mashariki,itaanza kutoa huduma ya upandikizaji uboho kwa watoto waliozaliwa na ugonjwa wa sikoseli ifikapo mwakani.
Akizungumza na Waandishi wa habari jijini Dodoma kuhusu mrejesho wa mpango ya utoaji wa huduma ya upandikizaji uboho katika kujibu magonjwa ya damu kama siko seli na kansa ya damu Mkurugenzi Mtendaji wa hopsitali hiyo, Dk Alphonce Chandika amesema “ Tumejipanga ifikapo mwaka 2020 kuanza kutoa huduma hii na tutaanza na huduma ya kuwasidia watoto wanaozaliwa wenye selimundu. Ugonjwa huu una mateso, maumivu makali, kuishiwa damu mara kwa mara, matibabu yake yana gharama na mtoto anatakiwa atibiwe maisha yake yote mara kwa mara.
Akiendelea kuelezea amesema hospitali yake imekuja na suluhisho la kudumu la kufanya upandikizaji kwa kuondoa uboho unaozalisha chebechembe za damu ambazo siyo nzuri na kuwekewa uboho mwingine ambao utazalisha damu isiyo na chemchembe za ugonjwa wa selimundu.
Dk Chandika amesema kwa mwaka huu watautumika kujengwa uwezo wa wataalamu ili tibahiyo iande kutolewa kwa mafanikio na bila kushindwa siku zijazo.
Akizungumzia kuhusu gharama, Dk Chandika amesema: “ Unapomfanyia upandikizaji wa uboho mgonjwa mmoja, inakuwa ni sawa na matibabu ambayo mgonjwa angepatiwa kwa miaka saba, ni rahisi kumtibu akapona kuliko kuishi kwa matibabu maisha yake yote
Naye dakatari bingwa wa watoto na magonjwa ya damu, Dk Shakiru Juma alisema mbali na faida ya kumpunguzia maumivu mgonjwa wa selimundu, pia itapunguza (carea) watanzania ambao wanavinasaba vya selimundu hivyo baadaye kuja kupata watoto wenye ugonjwa huo.
“ Kwa vile tunakwenda kubadili uboho wa mgonjwa mwenye selimundu kutapunguza carea ambao hawaumwi lakini wanavinasaba vya selimundi na ambao kwa watanzania kuna idadi kubwa ya carea hao,” amesema.
Naye mtaalamu wa upandikizaji wa uboho kutoka hospitali ya San Gerardo ya Italia, Profesa Cormelio Uderzo amesema hatua ya kuanza kutoa tiba hiyo itakisaidia nchi kuwa na kizazi kisicho na magonjwa.
“ Tiba hii ni muhimu ili kuwa na kizazi kisicho na magonjwa kwasababu upandikizaji uboho unatibu magonjwa mengi sana.
“ Tulikwenda Wizara ya afya na kuonana na katibu mkuu, unaona shauku yao ni kuwa tiba hii ianze leo au kesho, lakini ni lazima kujenga na kuimarisha timu itakayokuwa intaoa huduma hii kama vile madaktari, wauguzi wataalamu wa maabara na hata wale wanaokuwa kwenye benki ya damu ili tiba ikianza kutolewa itolewe kwa manufaa.”