Home | Terms & Conditions | Help

November 25, 2024, 9:36 am

NEWS: UBALOZI WA TANZANIA NCHINI ETHIOPIA KUCHUNGUZWA KWA WIZI

Dar es Salaam. Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Leo imeikabidhi Jalada Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) kulifanyia uchunguzi upotevu wa fedha katika Ubalozi wa Tanzania nchini Ethiopia.

Akikabidhi Jalada hilo leo Ijumaa Novemba 15, 2019 kwa Naibu Mkurugenzi Mkuu wa Takukuru, Brigedia Jenerali John Mbungo Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dk Faraji Mnyepe katika ofisi ndogo za wizara jijiji Dar es Salaam.

Hatua ya Wizara kukabidhi nyaraka hizo imekuja kutokana na jitihada za Serikali ya Tanzania inayoongozwa na Rais John Magufuli za kupambana na kuzuia rushwa pamoja na matumizi mabaya ya fedha za umma.

Uchunguzi huo unafanyika baada ya kubainika upotevu/matumizi mabaya ya fedha katika Ubalozi wa Tanzania nchini Ethiopia.

Kuhusu kiwango cha fedha kilichopotea Katibu Mkuu, Dk Mnyepe amesema kitajulikana mara baada ya Takukuru kukamilisha uchunguzi huo wa jalada walilokabidhi