Home | Terms & Conditions | Help

November 26, 2024, 12:52 am

NEWS: UBALOZI WA MAREKANI WAENDELEA KUIGANDA TANZANIA KESI YA KABENDERA

Kwa mara nyingine tena Ofisi za ubalozi wa Marekani na Uingereza nchini Tanzania zimeendelea kuiganda Serekali ya Tanzania kutokana na kesi ya mwanahabari maarufu wa Habari za kiuchunguzi nchini Tanzania, Erick Kabendera.

Image result for us embassy tanzania vs erick kabendera

Kama utakumbyWiki mbili zilizopita ofisi hizo mbili zilitoa tamko la pamoja juu ya kuhusu kile walichokiita "wasiwasi wa kuzorota kwa kwa haki za kisheria nchini Tanzania."

Katika tamko hilo, ofisi hizo mbili za ubalozi zinadai kuwa imedhihirika kwa zaidi ya mara moja watu kutiwa kizuizini kwa muda nchini Tanzania bila kupelekwa mahakamani na kubadilishiwa mashitaka na mamlaka zake za kisheria.

"Tuna wasiwasi hasa kwa tukio la hivi karibuni, jinsi ambavyo halikushughulikiwa kwa haki la kukamatwa, kuwekwa kizuizini na tuhuma za mashtaka ya mwandishi wa habari za uchunguzi Bw Erick Kabendera, ikizingatiwa ukweli kwamba alinyimwa haki ya kuwa na mwanasheria kwenye hatua za awali na kutiwa kizuizini kwake, ambapo ni kinyume cha sheria ya makosa ya jinai," inasema sehemu ya tamko hilo.

Jana Jumatano jioni, Agosti 21, 2019 ofisi hizo mbili kwamara nyingene tena kwa kupitia mitandao ya kijamii zilitoa ujumbe kuwa wanaendelea kufuatili kesi ya Kabendera.

"Tunaendelea kufuatilia kesi ya Erick Kabendera. Haki za kisheria ni haki ya raia wot, na kuhakikisha upatikatnaji wa haki hiyo ni wajibu wa serikali zote," unaeleza ujumbe ambao umechapishwa katika kurasa za twitter za Ubalozi wa Marekani na Balozi wa Uingereza nchini Tanzania Bi Sarah Cooke.

Kabendera alipandishwa kizimbani Agosti 5 na kusomewa mashtaka matatu ya ubadhirifu wa kiuchumi .

Katika mashtaka hayo Kabendera anatuhumiwa na kujihusisha na genge la uhalifu na uhujumu wa uchumi nchini Tanzania, shtaka la pili ni la kukwepa kulipa kodi ya zaidi ya milioni mia moja sabini za kitanzania.

Kosa la tatu ni la utakatishaji fedha zenye thamani ya zaidi ya millioni mia moja na sabini.

Kwa mujibu wa mashtaka yaliowasilishwa, Kabendera anadaiwa kuyatekeleza hayo baina ya Januari 2015 na Julai mwaka huu mjini Dar Es Salaam na kwa baadhi ya makosa anadaiwa kuyafanya kwa ushirikiano wa watu ambao hawakuwepo mahakamani.

Makosa yote hayana dhamana na Kabendera anaendelea kusota rumande.

Alifikishwa tena mahakamani Jumatatu wiki hii, lakini kesi ikaakhirishwa mpaka Agosti 30 baada ya upande wa mashtaka kudai hawajakamilisha upelelezi.