- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: TUME YA UCHAGUZI YATANGAZA TAREHE YA UCHAGUZI JIMBO LA LISSU
Dar es Salaam: Tume ya Taifa ya Uchaguzi Nchini (NEC) imetangaza ratiba rasmi ya kuanza mchakato wa uchaguzi mdogo wa ubunge wa jimbo la Singida Mashariki kuwa utafanyika Julai 31 mwaka huu.
Uchaguzi huo umeitisha mara baada ya Spika wa Bunge la Tanzania, Job Ndugai kulitangazia Bunge hilo kuwa Mbunge wa Jimbo hilo Tundu Lissu amepoteza sifa za kuwa mbunge huku akitoa sababu kuu mbili. Ndugai alisema kuwa Lissu hajajaza fomu za mali na madeni za maadili kwa viongozi wa umma pamoja na kutokutoa taarifa kwake (spika).
Kwamujibu wa Taarifa iliyotolewa leo Ijumaa Julai 05, 2019 na Mwenyekiti wa NEC Jaji Semistocles Kaijage amesema kutokana na barua ya Spika Ndugai kuwa Lissu kapoteza sifa ya kuwa mbunge kutokana na kushindwa kuwasilisha kwa Spika tamko la mali na madeni na kushindwa kuhudhuria mikutano saba mfululizo ya Bunge bila ruhusa ya Spika.
Jaji Kaijage amesema Spika Ndugai alizingatia matakwa ya kifungu cha 37 (1) (b) cha Sheria ya Taifa ya Uchaguzi sura ya 343, kutoa taarifa kwa Umma kuhusu uwepo wa Uchaguzi Mdogo wa Ubunge katika Jimbo la Singida Mashariki.
Amesema kwa kuzingatia Katiba ya nchi na Sheria ya Taifa ya Uchaguzi, ratiba ya uchaguzi huo utakuwa ni fomu za uteuzi wa wagombea zitatolewa kati ya Julai 13 hadi 18 mwaka 2019 na siku ya uchaguzi itakuwa Julai 31, 2019.
Pia Mwenyekiti huyo hakuacha kuvikumbusha vyama vya Siasa na wadau wote wa uchaguzi kuzingatia Sheria, Kanuni, Maadili ya Uchaguzi, Taratibu, Miongozo na Maelekezo yanayotolewa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi wakati wa kipindi chote cha uchaguzi huu mdogo.