- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: TUME YA UCHAGUZI NCHINI KENYA YASEMA MITAMBO YAKE IPO ULAYA
Nairobi: Tume kuu ya Uchaguzi nchini Kenya imesema kuwa mitambo yake ya kuhesabia matokeo halisi ya Uchaguzi Mkuu uliofanyika Agosti 8 mwaka huu, ipo barani Ulaya.
IEBC Kupitia kwa Wakili wake Paul Muite, imeambia Mahakama kuwa haijakataa kuwapa nafasi Mawakala wa upinzani kuangalia mitambo hiyo.
Hatua hii imekuja baada ya Mawakili wa Upinzani wanaomwakilisha Raila Odinga, anayepinga ushindi wa rais Uhuru Kenyatta kuiambia Mahakama kuwa, Tume ya Uchaguzi ilikuwa imekataa kutii agizo lake la kutaka Data zake za kuhesabia Uchaguzi kupekuliwa kwa pande zote mbili.
Siku ya Jumatatu, Mahakama iliruhusu pande zote kuangalia na kupitia mitambo ya Tume ya Uchaguzi na ripoti kuwasilishwa Mahakamani kufikia saa 11 jioni.Jaji Mkuu David Maraga, ameagiza kuwa uamuzi wa Mahakama hiyo uheshimiwe na ripoti kuwasilishwa hivi leo.
Siku ya Jumanne, upande wa utetezi umekuwa ukitoa ushahidi kupinga utetezi wa kiongozi wa upinzani NASA, Raila Odinga anayetaka matokeo yaliyompa ushindi kutupiliwa mbali.
Uamuzi wa mwisho unatarajiwa kutolewa siku ya Ijumaa huku kesi hiyo ikitarajiwa kumalizika hivi leo.