November 25, 2024, 12:47 pm
- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: TUME YA UCHAGUZI KENYA KUWAKUTANISHA WAGOMBEA URAIS LEO
Kenya: Tume ya Uchaguzi nchini Kenya IEBC, imepanga ikutane leo na wagombea urais kujadiliana kuhusu namna ya kupata zabuni mpya ya kuchapisha makaratasi ya kupigia kura ya urais.
Mkutano huu unafanyika ikiwa zimebaki siku 29 kabla ya Uchaguzi Mkuu nchini humo, na unakuja baada ya Mahakama kuu wiki iliyopita, kufuta zabuni iliyokuwa imetolewa hapo awali baada ya kubainika kuwa haikiuwa wazi na haikuwashirikisha wadau wote.Wananchi wa taufa hilo nao wanatarajiwa kutoa maoni yao kuhusu zabuni ya uchapishaji wa karatasi hizo, kwa mujibu wa katiba ya nchi hiyo kabla ya IEBC kutoa tangazo jipya.Hayo yakijiri rais wa Kenya Uhuru Kenyatta ameonya mahakama nchini humo akiitaka kutousaidia upinzani na kuhujumu uchaguzi unaokuja.
Uchaguzi wa urais utafanyika mwezi ujao ambapo uhuru Kenyatta anataka kuchaguliwa tena.
Ijumaa wiki iliyopita, mahakama kuu iliamrisha tume ya uchaguzi isichapishe makaratasi ya kupigia kura, baada ya upinzani kuwasilisha kesi mahakamani.