- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: TUME YA MAWASILIANO UGANDA YAVIFUNGA VITUO 13 VYA REDIO NA TV
Habari kubwa kutoka nchini Uganda nikwamba Tume ya Mawasiliano nchini humo imeagiza kufungwa kwa vituo 13 vya radio na televisheni pamoja na kufutwa kazi kwa baadhi ya wanahabari kwa kupotosha na kuchochea ghasia kwa kutangaza taarifa zilizo na ujumbe tofauti.
Tume hiyo inasema kuwa vyombo hivyo vya habari vilikiuka kanuni ya kifungu cha 31 ibara ya 4 ya sheria ya mawasiliano ya Uganda ya mwaka 2013. Japokuwa haikufafanua jinsi sheria hiyo ilivyokiukwa katika agizo lake kwa vyombo hivyo vya habari.
Tume inataka hatua dhidi ya wazalishaji vipindi, wahariri wa kuu na wasimamizi wa matangazo kusimamishwa kazi katika mda wa siku tatu.
“Hii ni kufuatia jinsi zinavyoshughulikia mada zinazorushwa hewani wakati wa matangazo ya moja kwa moja, Habari za hivi punde na Habari zingine kwa ujumla bila kuzingatia kanuni ,” iliongeza Tume ya UCC.
Chama cha wanahabari nchini Uganda (UJA) kimeelezea kughadhabishwa na hatua hiyo na kusema kuwa wanahabari karibu 30 wanakabiliwa na tishio la kufutwa kazi na hilo halitakuwa na athiri kwa taaluma zao tu bali mamilioni ya waganda watakosa huduma ya kupashwa habari.
Kwa upande mwingine, kuna madai kuwa huenda hiyo imetokana na mtangazo ya moja kwa moja ya kukamatwa na kushtakiwa kwa Mbunge wa Kyadondo Mashariki, Robert Kyagulanyi maarufu kama Bobi Wine.
Kyagulanyi kwa sasa anazuiliwa rumande na anatarajiwa kufikishwa tena mbele ya Hakimu Mkuu wa mahakama ya Buganda Road leo Alhamisi.