Home | Terms & Conditions | Help

November 24, 2024, 7:54 pm

NEWS: TRUMP AWAKEJELI WAPINZANI WAKE BAADA YA KUFUTIWA MASHTAKA

Rais wa Marekani Donald Trump amefurahia ushindi kwa kejeli nyingi mara tu baada ya kuondolewa mashtaka yaliyokuwa yakimkabili, ndani ya Ikulu ya Marekani amewaponda wapinzani wake wa kisiasa wakiongozwa na Spika wa Bunge Nancy Pelosi.

Trump akiwa ameshika gazeti lililoandika habari ya kusafishwa kwake


''Nimefanya makosa kwenye maisha yangu, nitakiri......lakini haya ndio matokeo, '' alisema huku akinyanyua gazeti lililokuwa na kichwa cha habari ''Trump hana hatia''.

''Tumepita kubaya, hatukutendewa haki.Hatukufanya kosa lolote,'' alisema Ikulu. ''Ulikuwa uovu, ilikuwa rushwa.''

'' Sasa tuna neno zuri. Sikufikiria kama litakuwa zuri namna hii, ''Linaitwa kusafishwa kabisa.''


Trump alishtakiwa na bunge la wawakilishi mwezi Desemba kwa matumizi mabaya ya madaraka na kulizuia Bunge kutekeleza majukumu yake, lakini hakukutwa na hatia siku ya Jumatano baada ya mchakato wa majuma mawili wa kesi dhidi yake kwenye bunge la seneti linalodhibitiwa na chama cha republican.

USA Amtsenthebungsverfahren | Abstimmung (picture-alliance/AP Photo/Senate Television)

Trump pia alieleza kuhusu uchunguzi uliokuwa ukifanyika kuhusu kampeni za uchaguzi wa mwaka 2016 na uhusiano na Kremlin.

''Ulikuwa upumbavu mtupu,'' alisema '' Hili suala halipaswi kutokea tena kwa rais atakayefuata.''

Trump alisema kuwa bado ana imani na chama cha Republican wakati huu wakielekea kwenye uchaguzi ujao wa mwezi Novemba.

Rais Trump aliwashukuru wabunge wa republican

Sherehe baada ya kusafishwa kwake kulitofautiana na rais Bill Clinton ambaye alihutubia mwaka 1999, alipoomba radhi kwa raia wa Marekani, baada ya kushtakiwa.

''Ninataka kusema tena kwa raia wa Marekani ninaomba radhi kwa kile nilichokisema na kwa mzigo mkubwa walioubeba wabunge na raia wa Marekani kwa ujumla,'' Bwana Clinton alieleza.

Alipokuwa akimaliza kuzungumza, Trump aliomba radhi kwa familia yake, kwa ''kupita kwenye misukosuko hiyo''.