- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: TRUMP ATUHUMIWA KUPENYEZA SIRI ZA KIJASUSI KWA URUSI
Washington: Rais wa Marekani Bw. Donald Trump ameingia kwenye shutuma nyingine nzito dhidi ya Urusi, Trump anadaiwa kupenyeza taarifa za kijasusi kuhusu operesheni iliyokuwa inapangwa dhidi ya wanamgambo wa kundi la Dola la Kiislamu IS kwa waziri wa mambo ya nje wa Urusi Bw. Sergei Lavrov.
Rais Trump akizungumza na waziri wa mambo ya njee wa Urusi Sergei Lavrov
Taarifa kutoka chombo cha habari cha Washington Post kinasema kimenukuu duru kutoka kwa maafisa wa zamani na wa sasa wa Marekani ambao wamesema Rais Trump alitoa taarifa nyeti za kijasusi kwa Lavrov na balozi wa Urusi nchini Marekani Sergey Kislyak wakati walipokutana kwa mkutano wiki iliyopita katika ikulu ya mjini Washington.Taarifa hizo Marekani ilipewa kutoka kwa mmoja wa mshirika muhimu wa Marekani anayehusika katika vita dhidi ya kundi hilo la kigaidi la IS, Ambapo anasema kuwa hakuipa Marekani ruhusa ya kuzitoa taarifa hizo zinazohusiana na mipango ya kigaidi ya kundi la wanamgambo wenye itikadi kali wa Dola la Kiislamu IS