Home | Terms & Conditions | Help

November 24, 2024, 1:38 pm

NEWS: TRUMP ATANGANZA HALI YA DHARURA MAREKANI

Rais wa Marekani Bw. Donald Trump ametangaza hali ya dharura nchini humo kutokana na tishio la kuenea kwa virusi vya corona, pamoja na upatikanaji wa karibu dola bilioni 50 kama msaada zaidi wa serikali ya shirikisho kupambana na ugonjwa huo.

Trump ametoa tangazo hilo katika mkutano na waandishi wa habari usiku wa kuamkia leo na kusema kwamba hali nchini humo inaweza kuwa mbaya zaidi na kwamba "wiki nane zinazofuata zinaweza kuwa mbaya sana".

Trump amekabiliwa na ukosoaji kutoka kwa baadhi ya wataalamu juu ya hatua za kujivuta na zisizo na ufanisi katika kushughulikia janga hilo. Hatua za hivi karibuni za Marekani zimekuja siku mbili baada ya Trump kupiga marufuku watu kuingia nchini humo hususan wakutokea Ulaya. Trump ambaye hapo awali alionekana kusimama kando ya afisa wa Brazil ambaye ameambukizwa COVID-19, amesema kwamba hata mwenyewe atafanyiwa vipimo haraka iwezekanavyo, lakini akaongeza kwamba hatojiweka karantini kwasababu hana dalili zozote.

Wakati huo huo shirika la afya ulimwenguni WHO, limesema Ulaya sasa ndio kitovu cha janga la virusi vya corona baada ya kesi za maambukizi nchini China ambako virusi hivyo vilianzia, kupungua. Kulingana na shirika hilo vifo duniani kote vimefikia watu 5,000. Televisheni ya taifa ya Iran imetangaza kwamba vikosi vya usalama vitaisafisha mitaa katika juhudi za kukabiliana na maambukizi zaidi. Kenya, Ethiopia, Sudan na Guinea nazo zimethibitisha visa vya kwanza vya COVID-19 na kuzifanya jumla ya nchi Afrika zilizoathirika kufikia 18.