- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: TITO MAGOTI AFUNGULIWA KESI YA UHUJUMU UCHUMI NA WENZAKE
Dar es Salaam. Mfanyakazi wa Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC) nchini Tanzania, Tito Magoti (26) na Mwenzake, Theodory Giyani (36), wamefikishwa katika mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Dar es Salaam wakikabiliwa na mashitaka matatu likiwemo utakatishaji fedha kiasi cha Sh. 17 milioni.
Magoti na Giyani, wamefikishwa mahakamani hapo leo Jumanne Desemba 24, 2019 na kusomewa mashtaka matatu likiwamo la utakatishaji fedha kiasi cha Sh17milioni.
Washtakiwa hao wamesomewa mashtaka yao mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu wa Mahakama hiyo, Janeth Mtega na jopo la mawakili wanne wa Serikali ya Tanzania.
Kabla ya kusomewa mashtaka hao, hakimu Mtega amesema washtakiwa hawatakiwi kujibu chochote kutokana na Mahakama ya Kisutu kutokuwa na uwezo wa kusikiliza kesi za uhujumu uchumi isipokuwa kwa kibali maalumu kutoka kwa mkurugenzi wa mashtaka (DPP).
Wakili wa Serikali Mwandamizi, Wankyo Simon amedai Magoti na Giyani, wanakabiliwa na kesi ya uhujumu uchumi namba 137/2019. Simon alidai katika shtaka la kwanza, Magoti na Giyani wanadaiwa kushiriki genge la uhalifu.
Kosa hilo wanadaiwa kutenda, katika tarehe tofauti kati ya Februari mosi na Desemba 17, 2019 jijini Dar es Salaam katika maeneo mbalimbali ya ndani ya nchi, ambapo Magoti, Giyani na wenzao ambao hawajafikishwa mahakamani, kwa makusudi walishiriki makosa ya uhalifu ikiwa ni kumiliki programu za kompyuta iliyotengenezwa mahususi kwa ajili ya kufanya uhalifu.
Wakili wa Serikali Mkuu, Faraja Nchimbi alidai katika shtaka la pili, washtakiwa hao na wenzao ambao bado hawajafikishwa mahakamani, wanadaiwa siku na eneo hilo, wanadaiwa kumiliki programu za kompyuta kwa lengo la kutenda kosa la uhalifu.
Katika shtaka la tatu, ambalo ni kutakatisha fedha, Wakili wa Serikali Mkuu, Renatus Mkude, alidai Magoti na Giyani, wanadaiwa kutenda kosa hilo kati ya Februari mosi na Desemba 17, 2019 katika Jiji la Dar es Salaam na maeneo mengine ndani ya nchi. Wanashtakiwa hao wanadaiwa katika tarehe hizo, walijipatia Sh17.35 milioni wakati wakijua fedha hizo ni zao tangulizi la kushiriki genge la uhalifu. Upelelezi wa kesi hiyo haujakamilika na hakimu Mtega ameahirisha kesi hiyo hadi Januari 7, 2020 itakapotajwa.