Home | Terms & Conditions | Help

November 27, 2024, 7:45 am

NEWS: TIRA WAPEWA SOMO

DODOMA: Makampuni, Madalali na Mawakala wa mamalaka ya usimamizi wa Bima (TIRA) nchini wameshauriwa kuendelea kutoa elimu ya bima ili kuwawezesha wananchi kuwa na ufahamu kuhusu umuhimu na maswala hayo.

Kauli hiyo imetolewa na katibu tawala wilaya ya Dodoma (Das) Jasinta Mboneno wakati akifungua mkutano wa makampuni, madalali na mawakala wa bima kwaniaba ya mkuu wa wilaya Dodoma mh, Christina Mndeme Uliofanyika mjini Dodoma.

‘’Elimu ya bima bado inahitajika kwani wananchi wachache ndio wenye ufahamu na niwale ambao wanatumia bima’’ amesema.

Pia amewataka watoa huduma wa mkoa wa Dodoma kuboresha huduma ili wa wananchi na wageni watakao kuja kuhudumiwa waone huduma ni bora wasitamani kufata huduma mikoa mingine .

‘’Ninawaomba wahudumie watu kwa ufasaha kwakuwalipa fidia zao kwa wakati muafaka’’amesema.

Akizungumza katika mkutano huo meneja wa mamlaka ya usimamizi wa bima (tira) Stella Lutaguza amesema wanahitaji kuongeza nguvu kwakutoa huduma stahiki zenye ubora wa hali ya juu ili kuendana na kasi ya serikali

Kwa upande wake mhasibu wa Tira kanda ya kati Rogers Msagati amewataka mawakala kufanya kazi kwa uweledi ili kuepuka usumbufu unaojitokeza kwa wateja.

‘’Sipendi kuona mteja anakuja ofisini kwangu kuleta malalamiko kuhusu kula hela yake ‘’amesema.

‘’Tujitahidi pia kufanya kazi zetu kwa ueledi na kwa kuzingatia taaluma zetu’’amesema.

wakizungumza na waandishi wa habari wadau wa bima kanda ya kati walisema bado juhudi zinaitajika katika kutoa elimu kwa wananchi ikiwa ni pamoja na kujitangaza

Moja ya wadau Charles balisbia alisema muamko wa wananchi kuhusu masuala ya bima mdogo kutokana na uelewa mdogo kwa wananchi.

‘’Elimu bado saivi tunajitahidi kutokana elimu kila sehemu ili wananchi waweze kupata elimu’’.

Hata hivyo wameweza kubainisha changamoto kuwa ni makapuni mengi kutofundisha vizuri,kukosa pesa za kuanzisha matangazo ya kutolea elimu kwa wananchi.