Home | Terms & Conditions | Help

November 26, 2024, 10:00 am

NEWS: TIMU YA AREA C YAUPA MKOA WA DOM HESHIMA

DODOMA: VIONGOZI wa soka mkoa wa Dodoma wametakiwa kuzimarisha timu za mkoa huo kwa kuanzisha mashindano ya mara kwa mara ili kuweza kunufaika na uwanja wa mpira wa kimataifa unaonjengwa mkoani hapa.

Akizungumza na waandishi wa habari katika ofisi ya mkuu wa mkoa leo mjini Dodoma mwenyekiti wa kamati ya michezo ambaye pia ni katibu tawala wa mkoa Rehema Seif Madenge wakati wa kutoa zawadi ya shukurani kwa mkuu wa mkoa wa huo.

Amesema kutokana na kuwa na changamato nyingi za ukosekana ya fedha katika timu zetu za mkoa ni muhimu kuanzisha mashindano ya mara kwa mara ambayo yatasaidiakila Kila timu kujipatia kipato ambacho kisaidia kujiendeleza.

‘’Kwanini tusitengeneze namna ya mashindano au michezo ya mara kwa mara na timu nyingine ilitusaidia kujiingizia kipato maana yake unapoomba kuna kuchokwa ‘’amesema.

‘’ Namhafahamu sasa hivi kuna uwanja wa kimataifa unajengwa hapa sasa isije ikawa timu za kutoka nje ya mkoa ndo zikaja kucheza hapa kwetu wakati mkoa wa dodoma hakuna timu za kucheza’’ amesema Madenge.

Hata hivyo ameipongeza timu ya AREA C Dodoma kwa kuupatia mkoa wa dodoma heshimu

Timu ya AREA C Dodoma ilibuka kidedea kuwa mshindi wa ligi daraja la pili mkoa baada ya kutoka daraja la tatu siku chache baada ya mashindano ya ligi yalifanyika katika mkoa wa dodoma na mikoa mbalimbali ukiwemo mkoa wa tabora