- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: TFF YAMTIMUA KOCHA WA TAIFA STARS EMMANUEL AMUNIKE
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limemfukuza Kocha wa Timu ya Taifa ya Tanzania “Taifa Stars” Emmanuel Amunike baada ya kuwa na mwendondo mbovu kwenye mashindano ya Afrika ya AFCON ambapo taifa stars ilitoka patupu(bila alama hata moja) katika mashindano hayo.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa leo Jumatatu July 8, 2019 na TFF imesema kuwa wamefikia makubaliano na kocha huyo ya kuendelea kuhudumu kama kocha mkuu
"tumefikia makubaliano ya pamoja kusitisha mkataba baina yetu" imesema sehemu ya taarifa ya TFF
"TFF itatangaza Kocha wa muda atakaekiongoza Kikosi cha Timu ya Taifa kwa mechi za CHAN.
Makocha wa muda watatangazwa baada ya Kamati ya Dharura ya Kamati ya Utendaji (Emergency Committee) itakapokutana Julai 11,2019.
Mchakato wa kutafuta Kocha mpya umeanza mara moja."
Taifa Stars iliondoka Misri bila hata pointi moja, ikishika mkia kwenye kundi hilo, nyuma ya jirani zao, Kenya waliovuna pointi tatu, ingawa nao pia wanarejea nyumbani, huku Senegal iliyomaliza na pointi sita katika nafasi ya pili ikiungana na Algeria iliyokusanya pointi tisa kwenda hatua ya 16 Bora.
Taifa Stars ya kocha Emmanuel Amunike imeshindwa kuvunja rekodi ya kikosi cha mwaka 1980 kilichoshiriki fainali hizo mjini Lagos, Nigeria ambacho angalau kiliambulia pointi moja baada ya sare na Ivory Coast ya 1-1, kikitoka kufungwa 2-1 na Misri na 3-1 na wenyeji, Nigeria.