- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: TFDA YAFUTA TOZO 9 NA KUBADILISWA JINA KUWA TMDA
Mamlaka ya Chakula na Dawa nchini tanzania (TFDA) imefanikiwa kufuta tozo 9 ilizokuwa ikiwatoza wateja wake, pia kuanzia tarehe 1 julai 2019 italazimika kubadili jina na majukumu yake kama TFDA na kuwa mamlaka inayosimamia madawa na vifaa tiba pekee (Tanzania Medicines and Medical Devices Authority (TMDA)) na majukumu iliyokuwa nayo kama TFDA yatafanywa na Shirika la viwango Tanzania (TBS).
"Katika kutekeleza Blueprint ya kuboresha mazingira ya biashara na uwekezaji nchini TFDATanzania imefuta tozo 9 na kuhamisha majukumu ya udhibiti wa chakula na vipodozi kwenda TBS. Aidha, Gcla1895 imefuta tozo 8, kupunguza tozo 10 na kuanza kutoza kwa Tsh badala ya USD..1" amesema Naibu wa Afya Dkt Faustine Ndugulile
"Hivyo, kuanzia tarehe 1 Julai, 2019 Mamlaka ya Chakula na Dawa TFDATanzania itajulikana kama kama Tanzania Medicines and Medical Devices Authority (TMDA). Taasisi hii itasimamia masuala ya dawa na vifaa tiba pekee. Majukumu udhibiti ya chakula na vipodozi yatafanywa na TBS." aliongeza Dkt Faustine Ndugulile kupitia ukurasa wake wa twitter
Jumatano Juni 26, 2019 na Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Dk Ashatu Kijaji wakati akiwasilisha bungeni muswada wa sheria ya fedha mwaka 2019 Serekali ilipendekeza marekebisho ya sheria ya viwango sura 130 ili kuhamisha majukumu ya kusimamia masuala ya chakula na vipodozi kwa Shirika la Viwango Tanzania (TBS) kutoka Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA) ambayo inasimamia majukumu hayo
“Inapendekeza kufanya marekebisho ya Sheria ya Chakula, Dawa na Vipodozi sura ya 219 ili kuiondolea TFDA jukumu la kusimamia chakula na vipodozi.” “Aidha marekebisho haya yanapendekeza kubadilisha jina la taasisi ya TFDA ili kuwa TMDA (Mamlaka ya Dawa na Vifaa Tiba) ambayo itaendelea kusimamia dawa, vifaa tiba na vitendanishi ili kuongeza ufanisi katika eneo hili,” amesema Dk Mpango.