- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: TEUZI 6 MUHIMU ZA RAIS MAGUFULI
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli leo tarehe 31 Januari, 2020 amefanya uteuzi wa viongozi mbalimbali wa Wizara, Mahakama, Mikoa na Majeshi.
Katibu Mkuu Kiongozi, Mhe. Balozi John Kijazi amewataja walioteuliwa kama ifuatavyo;
Wizara.
1. Mhe. Rais Magufuli amemteua Bi. Mary Gasper Makondo kuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi. Kabla ya uteuzi huo Bi. Mary Gasper Makondo alikuwa Kamishna wa Ardhi katika Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi. Anachukua nafasi ya Bi. Doroth Mwanyika ambaye amestaafu.
2. Mhe. Rais Magufuli amemteua Dkt. Hassan Abbas kuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo. Kabla ya uteuzi huo Dkt. Hassan Abbas alikuwa Mkurugenzi wa Idara ya Habari Maelezo. Anachukua nafasi ya Bi. Suzan Mlawi ambaye amestaafu.
3. Mhe. Rais Magufuli amemteua Prof. Riziki Silas Shemdoe kuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda na Biashara. Kabla ya uteuzi huo Prof. Riziki Silas Shemdoe alikuwa Katibu Tawala Mkoa wa Ruvuma. Anachukua nafasi ya Prof. Joseph Buchweishaija ambaye amestaafu.
4. Mhe. Rais Magufuli amemteua Bi. Zena Ahmed Said kuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati. Kabla ya uteuzi huo Bi. Zena Ahmed Said alikuwa Katibu Tawala Mkoa wa Tanga. Anachukua nafasi ya Dkt. Hamis Mwinyimvua ambaye amestaafu.
5. Mhe. Rais Magufuli amemteua Bw. Christopher Kadio kuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi. Kabla ya uteuzi huo Bw. Christopher Kadio alikuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Mwanza. Anachukua nafasi ya Mej. Jen Jacob Kingu ambaye ameteuliwa kuwa Balozi.
6. Mhe. Rais Magufuli amemteua Bw. Leonard R. Masanja kuwa Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati. Kabla ya uteuzi huo Bw. Leonard R. Masanja alikuwa Kamishna wa Umeme na Nishati Mbadala.