Home | Terms & Conditions | Help

November 25, 2024, 6:44 pm

NEWS: TCRA YATOA ELIMU KWA WATUMIAJI WA SIMU ZA MKONONI

DODOMA: MAMLAKA ya mawasiano Tanzania (TCRA)imetoa ufafanuzi wa jinsi ya kutumia namba ya simu ya awali kutoka mtandao mmoja wa simu ya mkononi na kuhamia katika mtandao mwingine.

Mbali na kutoa ufafanuzi huo uongozi wa TCRA umesema kuwa mteja ambaye anatakiwa kuhamia mtandao mwingine hatapata huduma hiyo kama anadaiwa deni la aina yoyote katika line yake ya awali.

Hayo yamebainishwa leo mjini hapa na mhandisi mwandamizi wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania [TCRA] Francis Mihayo, alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari wakati akitoa elimu kuhusu huduma ya kuhamia mtandao mwingine wa simu bila kubadili namba ya simu ya kiganajani .

Amesema kama wananchi hawataridhishwa na huduma ya mitandano hiyo hatua ya kwanza ni kutoa tarifa kwa mtoa huduma, kama tatizo lake halija tatuliwa afike kwenye mamalaka husika[TCRA].

Mhandisi Mihayo ameeleza kuwa masharti ya kuhamia mtandao mwingine ni hutaweza kuhama na nambaambayo imefungiwa au kusimamishiwa huduma,huwezi kuhama iwapo una mkopo wa aina yoyote ile (muda wa maongezi au pesa mtandao) kutoka kwa mtoa huduma hapa wako hapa nchini.

Pia ameongeza kuwa utaratibu wa kuhama ni pamoja na mhudumu atakutaka uajaze fomu maalumu ya maombi amabapo itatakiwa kuwa na kitambulisho chenye picha yako,kitambulisho cha taifa,kadi ya mpiga kura , leseni ya udereva au pasipoti au kitambulisho chochote rasmi kinachotambulika.

Amesema huduma ya simu inaaza kufanya kazi kwa muda wa siku 30 tangu kutoka mtandao moja ulioamua kujitoa na kujiunga na mtandao mwingine.

Mbali na hili mhandisi Mihayo amesema mteja wa simu ya kiganjani anao uwezo wa kuhamia mitandao mingine mara 12 kwa mwaka.