Home | Terms & Conditions | Help

November 24, 2024, 4:28 pm

NEWS: TANZANIA YAPATIWA MKOPO WA SH. TRILIONI 3.3 KWA AJILI YA RELI (SGR)

Serekali ya Tanzania imepokea Mkopo nafuu wa dola za Marekani bilioni 1.46, sawa na shilingi za Tanzania Tril. 3.3 kutoka benki ya Standard Chattered (Tanzania) kwa ajili ya ujenzi wa Reli kwa Kiwango cha Kimataifa (SGR), kipande cha Morogogoro hadi Makutupora, mkoani Singida,

Mkopo huo umesainiwa leo Jijini Dar es Salaam 13 Februari, 2020 na Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb) na Mkurungenzi wa Banki ya Standard Chattered (Tanzania) Sanjay Rughani.

Wadau mbalimbali waliohusika na kutoa mkopo huo pamoja na utekelezaji wa Ujenzi wa Mradi wa Reli kwa kiwango cha Kimataifa (SGR), alikuwepo Balozi wa Denmark nchini Tanzania Mhe. Mette Norgaard Dissing-Spandet (wa pili kushoto) na Balozi wa Sweden nchini Tanzania Mhe. Anders Sjoberg (wa nne kushoto) baada ya kusainiwa kwa makubaliano ya mkopo nafuu wa dola za Marekani bilioni 1.46, sawa na shilingi za Tanzania Tril. 3.3 ambazo Benki hiyo imetoa kwa ajili ya ujenzi wa Reli hiyo.

mradi mkubwa wa ujenzi wa reli ya kisasa ya Standard Gauge - unaendelea. Reli hiyo inayoanzia bandari ya Dar es Salaam hadi mji mkuu wa Dodoma na baadaye hadi nchi za jirani za Rwanda Burundi na DR Congo.

Mradi huo umeelezwa kuwa mkubwa zaidi katika miundombinu kufanyika miaka ya hizi karibuni na manufaa yake kiuchumi kuwa makubwa si kwa Tanzania tu bali hata nchi za jirani.

Awamu ya kwanza yenye umbali wa KM zaidi ya 400 kutoka bandari ya Dar es Salaam hadi Dodoma unatarajiwa kukamilika 2019

Lakini lengo hasa ni kuziunganisha nchi jirani kama Rwanda, Burundi, Uganda na DR Kongo na reli hiyo.

Lakini Nchi kama Ethiopia bado haijanufaika na reli yake mpya kuelekea Djibouti katika kiwango ilichokitarajia wakati wa ujenzi, wengi wanatahadharisha juu ya matarajio ya Tanzania kwamba wakati manufaa ya kiuchumi yanaonekana kuwa wazi hivi sasa, lolote linawezekana.

Ujenzi

Kadhalika, kuna uwezekano matunda yasifikie kiwango kinachotarajiwa au yakachelewa kuonekana kinyume cha matarajio ya wengi.