- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: TANZANIA YAPATA KIFO CHA KWANZA CHA CORONA
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu leo amethibitisha kifo cha kwanza cha mgonjwa wa virusi vya corona ambaye ni mwanamume aliyekuwa akitibiwa katika Hospitali ya Taifa ya Mloganzila.
Kwa mujibu wa taarifa ya Waziri Ummy iliyotolewa leo Asubuhi Machi 31 amesema mgonjwa aliyepoteza maisha ni Mtanzania mwenye umri wa miaka 49 aliyekuwa akipatiwa matibabu katika Hospitali ya Taifa ya Mloganzila.
“Nasikitika kutangaza kifo cha kwanza cha mgonjwa wa Covid -19 hapa nchini kilichotokea alfajiri ya leo tarehe Machi 31, wakati akiendelea kupatiwa matibabu katika kituo cha Mloganzila Dar es salaam.
“Marehemu ni Mtanzania mwenye umri wa miaka 49 ambaye pia alikuwa akisumbuliwa na maradhi mengine, tunamwomba Mwenyezi Mungu ailaze roho ya marehemu mahali pema peponi na tunatoa pole kwa ndugu hasa wa marehemu,” amesema Waziri Ummy.
Hadi sasa jumla ya wagonjwa waliopata maambukizi ya Covid-19 nchini ni 19, aliyepona ni mmoja na aliyefariki dunia ni mmoja.