- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: TANZANIA NA CHINA WASAINI MAKUBALIANO YA TAALUMA YA ICT
DODOMA: Katibu Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Dkt. Leonard Akwilapo leo amesaini makubaliano na Jamuhuri ya Watu wa China - (MOU) ya kuwasafarisha wanafunzi Kumi kutoka Tanzania kuelekea nchini China kwa ajili ya kujifunza Taaluma ya Mawasiliano ya kompyuta, ICT - kupitia Makao makuu Huawei ya nchini humo katika kipindi cha wiki tatu.
Akizungumza na wanafunzi wanaotarajiwa kuhudhuria mafunzo hayo leo mjini Dodoma, Dkt. Akwilapo amewataka wanafunzi hao kuhakikisha wanakwenda kujifunza, na kuangalia Maendeleo ya kompyuta ili waweze kuja kuendeleza ufundi na ujuzi wa Teknolojia watakaokuwa wameupata nchini China.
Hii ni mara ya Pili kwa Makao makuu ya Huawei ya nchini China kusafirisha wanafunzi kwenda nchini humo kwa ajili ya mafunzo hayo ya kompyuta lengo likiwa ni kuwajengea vijana uwezo katika mawasiliano .