Home | Terms & Conditions | Help

November 24, 2024, 7:42 pm

NEWS: TANZANIA HAINA MGONJWA WA CORONA.

DODOMA: Mpaka sasa Tanzania haina Mgonjwa wala muhisiwa wa ugonjwa unaosababishwa na kirusi cha Coromna (Hona kali ya mafua) hata hivyo kutokana na mwingiliano mkubwa uliopo hasa kibiashara na kijamii kati ya Tanzania na nchi za bara la Asia ikiwemo nchi ya China nchi inakuwa katika hatari pia ya ugonjwa huo.


Haya yamesemwa leo na Waziri wa Afya, maendeleo ya jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Ummy Mwalimu wakati akitoa tarifa kwa umma kuhusu mwenendo wa ugponjwa huo jijini hapa.


“Ugonjwa huu unasababiswa na kirusi jamii ya Corona na ni kipya “Novel (New) Corona virus 2019” (2019-nCOV) ambacho ni tofauti na virusi vingine vya jamii hiyo ambavyo viliwahi kusababisha milipuko ya ugonjwa uliojulikana kama ‘SARS-CoV’ mwaka 2003 na MERS-CoV Corona Virus mwaka 2013”.Amesema Waziri Ummy.

Aidha, waziri Ummy amesema ugonjwa huo huambukizwa kwa njia ya hewa kwa kuingiwa na majimaji yenye virusi kutoka mtu mmoja kwa njia ya kukohoa au kupiga chafya au kwa kugusa majimaji au makamasi kutoka kwa mgonjwa aliyethibitishwa kuwa na dalili za ugonjwa huo na dalili huanza kuonekana kati ya siku moja hadi kumi na nne tangu kupata maambukizo.

Hata hivyo ametaja dalili za ugonjwa huu ni pamoja na Homa, mafua, kuumwa kichwa, mwili kuchoka, kikohozi, kubanwa mbavu, maumivu ya misuli, vidonda vya koo, mapafu kuathirika, kupumua kwa shida na hata kifo.

“Ugonjwa huu hauna chanjo wala tiba ya moja kwa moja, hivyo kama yalivyo magonjwa mengine yanayosababishwa na virusi, matibabu hufanyika kwa kuzingatia dalili zilizopo na ufuatiliaji wa karibu” Amesisitiza Waziri Ummy.

Wakati huo huo waziri huyo amewashauri wananchi kuchukua hatua ili kujikinga na ugonjwa huo ikiwemo kuzingatia kanuni za afya na usafi ikiwa ni pamoja na kukaa mbali na mtu mwenye dalili za mafua mwenye historia ya kusafiri katika nchi zilizokumbwa na mlipuko na kufunika mdomo na pua wakati wa kukohoa kwa kitambaa safi au nguo uliyovaa sehemu za mikono

“Kutokana na mwenendo na kasi ya kusambaa kwa ugonjwa huo kipindi hiki cha mlipuko, Wizara inashauri kusubiri na kuepuka safari zisizo za lazima kwenda kwenye maeneo yaliyoathirika na inapolazimu kusafiri basi wapate maelezo ya kitaalamu kabla ya kuondoka nchini pamoja na kuepuka kugusana na mgonjwa mwenye dalili za magonjwa ya njia ya hewa”.

Vile vile wananchi wanatakiwa kutoa taarifa ya uwepo wa mtu mwenye dalili zinazohiswa kuwa za ugonjwa huu kwenye kituo cha huduma za afya kilicho karibu nawe au piga simu namba 0800110124 au 0800110125 bila malipo.