- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: TAKWIMU SAHIHI NI NYENZO MUHIMU KATIKA KUFANIKISHA KAZI ZA WAHUDUMU WA AFYA.
MOROGORO: Imeelezwa kuwa matumizi ya takwimu sahihi ni nyenzo muhimu katika kufanikisha kazi na majukumu ya kila siku ya Wahudumu wa Afya Ngazi ya Jamii.
Hayo yamebainishwa Mkoani Morogoro na Mkurugenzi Msaidizi wa huduma za lishe kutoka Ofisi ya Rais TAMISEMI Luitfrid Nnally wakati wa ufunguzi wa mafunzo ya kuwajengea uwezo Wakufunzi kutoka vyuo vya Afya (HTis) vinavyotoa mafunzo ya Wahudumu wa Afya ngazi ya jamii pamoja na Waratibu wa Mikoa 12 na Halmashauri 25 kuhusu kitabu cha Mtua Namba 3.
Nnally amesema katika kufanikisha matumizi sahihi ya nyenzo na kuchukua taarifa jambo la takwimu sahihi ni la msingi.
“Watoa huduma wa Afya ngazi ya jamii ili waweze kutumia vizuri nyenzo na kuweza kuchukua taarifa kwa ajili ya kusaidia mambo mbalimbali zitakazosaidia kuwaratibu vizuri na hizi taarifa zikiwa safi sana zitatuwezesha kutoa maamuzi ambayo yanazingatia takwimu, maana yake mkiwafundisha vizuri watazingatia taratibu zote za kufanya kazi na kurahisisha ufuatiliaji hata kujua magonjwa yapo wapi, msimu gani , maeneo gani na hiyo inasaidia sana kupeleka rasilimali mahali sahihi panapohusika “amesema.
Aidha, ametumia fursa hiyo kuishukuru Serikali ya awamu ya sita chini ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuwezesha kufanikisha Mpango jumuishi wa Wahudumu wa Afya ngazi ya jamii uliozinduliwa tarehe 31, Januari, 2024 na Makamu wa Rais Dkt. Philip Mpango ambapo sasa Wahdumu wa Afya ngazi ya jamii wanapata mafunzo katika vyuo mbalimbali vya afya katika mikoa 11 na halmashauri 23 za mwanzo katika kuhakikisha Watanzania wanakuwa na afya bora .
“Takwimu ndio zinazotuunganisha sisi na dunia, Tanzania na WHO, na takwimu hutumika kutengeneza sera za Wizara na ni mstari wa mbele kutengeneza takwimu na Mhudumu wa Afya ngazi ya jamii asitumie muda mwingi kurekodi atoe huduma lakini ahakikishe kinachorekodiwa ni sahihi na matumaini yetu kuwa Wahudumu wa Afya ngazi ya jamii watasaidia sana kwenye eneo la kinga”amesema.
Kwa upande wake Mkufunzi wa Kitaifa wa Mafunzo ya Mtua Namba 3 Denis Kashaija amesema Wahudumu wa Afya Ngazi ya Jamii ni watu muhimu hivyo kupitia mafunzo hayo yatarahisisha upatikanaji wa takwimu sahihi huku Mwalimu Mkufunzi wa Mafunzo Sister Rucy Ifunya akisema takwimu hurahisisha kufanikisha mipango sahihi.