- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: TAKUKURU YAZUA NGUMZO KWA TAASISI 17
DODOMA: WAZIRI wa Fedha na Mipango, Dk. Philipo Mpango ameigiza Taaasisi ya Kupambana na Kuzuia Rushwa(TAKUKURU) mara moja kuzifikisha taasisi 17 zenye miradi 33 ambazo zimebainika kuwa na viashiria vya rushwa.
Pia imesema kamwe serikali haitavumilia kuona taasisi hizo zinafanya manunuzi ya hovyo na kufuja fedha za watanzania na hakuna jiwe ambalo wataacha kuligeuza katika serikali ya Awamu ya Tano.
Taarifa za kuwepo kwa viashiria hivyo vya rushwa zimebainika kufuatia ripoti ya thathimini ya utendaji kazi wa PPRA kwa mwaka wa fedha 2016/17, iliyokabidhiwa kwa waziri wa fedha leo.
Akizungumza baada ya kupokea ripoti hiyo, Dk. Mpango amesema, taarifa hiyo waliyoipokea ni muhimu kwani zaidi ya asilimia 70 ya fedha zote za umma zinatumika kwa ajili ya kununua vifaa vya serikali na taasisi zake.
Waziri Mpango, akizungumza kuhusu wizara yake kutajwa katika viashiria hivyo vya rushwa amesema ni sahihi kabisa, kwani wao wanahitaji kuwa mfano.
Awali akikabidhi ripoti hiyo ambayo ni ya 11 tangu kuanzishwa kwa PPRA, Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya PPRA Dk. Matern Lumbunga, alisema ukaguzi uliofanywa na PPRA ulipima uwezekano wa uwepo wa rushwa ktika taasisi au miradi husika ambapo thamani ya jumla ya viashiria vya rushwa inaonesha kwamba miradi 33 katika taasisi 17 ilibainika kuwa na kiwango kikubwa cha viashiria vya rushwa.
Alizitaja taasisi hizo kuwa ni pamoja na Mamlaka ya Majisafi na Taka za Moshi(MUWASA), Mwanza(MUWASA), Arusha(Auwasa) pamoja na halmashauri za Wilaya ya Msalala, Kibondo na Moshi.
Taasisi nyingine ni Taasisi ya Sayansi na Teknolojia ya Nelson Mandela, Wizara ya maji na Umwagiliaji, Chuo cha UfundI Arusha, Halmashauri ya Mji wa Kahama, Hospitali ya Taifa ya Muhimbili na Taasisi ya Uhasinu Arush(IAA).
Nyingine ni Ofisi ya Katibu Tawala mkoa wa Kilimanjaro, Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Mamlaka ya Mapato Tanzania(TRA), Halmashauri ya Mji wa Masasi pamoja na Kituo cha Kimataifa cha Mikutano cha Arusha(AICC).
Amesema, mbali na kufanya uchunguzi wa kawaida PPRA ilifanya uchunguzi wa tuhuma za ukiukwaji wa sheria na taratibu za manunuzi, ambapo katika mwak wa fedha 2016/17 ilifanya uchunguzi wa tuhuma nane zilizohusu mikataba 10 ya manunuzi iliyokadiriwa kuwa na thamani ya sh. bilioni 280, iliyotekelezwa na taasisi nane uchunguzi uliotokana na maagizo kutoka mamlaka za juu na taasisi zenyewe.
Amezitaja taasisi hizo kuwa ni Mamlaka ya Mapato Tanzania(TRA), Taasisi ya Mifupa(MOI), Mamlaka ya vitambulisho vya Taifa(NIDA), Shirika la Bima la Taifa(NIC),Mamlaka ya Udhibiti wa Mawasiliano(TCRA), Mamlaka ya Usafiri wa Anga(TCCAA), Wizara ya Fedha na Mipango na Halmashauri ya Wilaya ya Kondoa.
Alisema, kwa upande mwingine taasisi 81 kati ya 112 zilifanyiwa ukaguzi wa kupima thamani ya fedha, na jumla ya mikataba ya miradi 345 ilikaguliwa ambapo miradi 87 ilipata alaza za kiwango cha kati/ kawaida na miradi saba ilipata alama za kiwango kisochoridhisha.
Mwenyekiti huyo alibainisha kuwa, miradi iliyopata kiwando kisichoridhisha inajumuisha miwili ya ujenzi wa majengo yenye thamani y ash. Milioni 201.542, ambapo mradi mmoja wa ujenzi wa barabara ilikuwa na thamani ya sh. milioni 146.92 na miradi miwili ya ujenzi yenye thamani ya sh. milioni 405.63.
“Minine ni mmoja wa huduma za ushauri wa kitaalam wenye thamani ya sh. milioni 25.46 na mradi mmoja wa usambazaji wa maji wenye thamani ya sh.bilioni 1.59.
Kuhusu ukaguzi wa kupima upatikanaji wa thamani halisi ya fedha alisema, ulibaini malipo yenye utata katika taasisi tatu ambapo kiasi cha sh. Milioni 483.44 zililipwa kwa wakandarasi kwa kazi ambazo hazikuwa zimefanyika.
Alizitaja taasisi hizo kuwa ni pamoja na Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii(NSSF), Kampuni ya simu Tanzania (TTCL) na Halmashauri ya Wilaya ya Kwimba iliyoko mkoani Mwanza.