Home | Terms & Conditions | Help

November 26, 2024, 12:22 pm

NEWS: TAKUKURU YAWASAKA WAMILIKI MEIS INDUSTRIES KWA WIZI WA BIL 46

Dar es Salaam. Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa nchini(Takukuru) inawatafuta wamiliki wa Kampuni ya Meis Industriesltd wanaodaiwa kutoroka na fedha kiasi cha Sh46 bilioni ambazo zilikuwa ni mkopo kwa ajili ya kujenga kiwanda cha saruji mkoa wa Lindi. Amewataja wahusika wa kampuni ya Meis ambao hawajapatikana na wanaendelea kutafutwa ni Islam Balhabou, Merey Awadh Saleh, Sabri Kuleib na Abdallah Bin Aliya.

Akizungumza na waandishi wa habari leo Jumanne Juni 18,2019 Naibu Mkurugenzi Mkuu wa Takukuru, Brigedia Jenerali John Mbungo amesema wamebaini kampuni ya Meis ilikabidhiwa fedha hizo kama mkopo mwaka 2011 kutokana na sehemu ya fedha za uwekezaji zilizotolewa na Serikali ya Libya kwa Serikali ya Tanzania.

"Mwaka 2009 Serikali zote mbili zilisaini mkataba wa nyongeza ambao uliitaja kampuni ya Meis kama kampuni itakayopewa kiasi cha dola 20,000,000 kwaajili ya uwekezaji wa ujenzi wa kiwanda cha saruji eneo la Machole Mkoani Lindi,” amesema Brigedia Mbungo.

Amewataja wahusika wa kampuni ya Meis ambao hawajapatikana na wanaendelea kutafutwa ni Islam Balhabou, Merey Awadh Saleh, Sabri Kuleib na Abdallah Bin Aliya.