Home | Terms & Conditions | Help

November 26, 2024, 4:44 am

NEWS: TAKUKURU YAMTIA MBARONI OFISA WA TRA KWA RUSHWA

Taasisi ya Kupambana na Kuzuia na Rushwa (Takukuru), Mkoa wa Ilala inamshikilia Ofisa wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Bw. Elias Yunus kwa tuhuma za kuomba Rushwa ya Sh milioni 50 na kupokea Dola za Marekani 1,000 kwa ahadi ya kutaka kumsaidia mfanyabiashara aliyetaka kukwepa kodi na kujaza taarifa za uongo.

Akizungumza na waandishi wa habari leo Ijumaa Agosti 2, Kaimu Mkuu wa Takukuru Mkoa wa Ilala, Enock Ngailo amesema mtuhumiwa huyo alikamatwa baada ya kuomba ushwa kwa mfanyabiashara Raia wa Uturuki (jina limehifadhiwa), ambaye ni Mkurugenzi wa Kampuni ya HEM Heavy Equipments Company Ltd.

Ngailo amesema ofisa huyo alitengeneza mazingira ya rushwa baada ya mfanyabiashara huyo kutoa taarifa za uongo katika usajili wa mtambo aliouingiza kutoka nje ya nchi kwa lengo la kukwepa kodi.

“Kinyume na kifungu cha Sheria ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Na. 11 ya mwaka 2007, mtuhumiwa aliomba rushwa ya Sh milioni 50 na tayari amepokea Dola za Marekani 1,000 ili aweze kumsaidia mfanyabiashara huyo.

“Uchunguzi wa Takukuru umebaini mtuhumiwa aliomba rushwa hiyo na baada ya majadiliano alipunguza kiasi hicho na kufikia Sh milioni 35 kwa masharti ya kupewa fedha hizo zikiwa katika Dola za Marekani (Dola 17,000)