- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: TAKUKURU YAMSHIKILIA AFISA TANESCO KWA KUOMBA RUSHWA YA NGONO
Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) mkoani Mtwara leo Jumanne Julai 9, imemkamata Ofisa Utumishi wa Shirika la umeme Tanzania (Tanesco), Jumanne Songoro kwa tuhuma za kuomba rushwa ya ngono kwa mtumishi mwenzake ili ampangie majukumu mazuri ya kazi Katika kitengo cha kudumu.
Kamanda wa Takukuru mkoa wa mtwara Stephen Mafipa amesema leo julai 9 kuwa afisa huyo amekamatwa baada ya kupata taarifa kutoka kwa mlalamikaji na baada ya uchunguzi waliweka mtego na kufanikiwa Kimkamata mtuhumiwa.
Mafipa amesema katika mtego huo walifanikiwa kumkuta mlalamikaji akiwa na afisa huyo kwenye moja ya nyumba za wageni ambapo uchunguzi umebaini kuwa mtuhumiwa alianza kushawishi rushwa ya ngono tangu Desemba 2018 hadi juni 4 mwaka huu ambapo mlalamikaji aliwasilisha malalamiko hayo Takukuru kwa lengo la kupata msaada.
“Kwa majibu wa mlalamikaji mtuhumiwa alitaka rushwa hiyo kutoka kwa mtmishi mwenzake ili ampangie majukumu mengine ya kazi Katika kitengo cha kudumu kulingana na kiwango cha elimu baada ya kubadilishiwa majukumu ya awali kufuata maagizo kutoka makao makuu ya Tanesco,” amesema Mafipa.
Mtuhumiwa atafikishwa mahakamani na kufunguliwa mashtaka chini ya kifungu cha 25 cha sheria ya kuzuia na kupambana na rushwa baada ya kukamilisha taratibu za kisheria.