Home | Terms & Conditions | Help

November 26, 2024, 11:18 pm

NEWS: TAKUKURU YAMNG’ANG’ANIA SIMPI KONDOA.

KONDOA DODOMA: Mwenyekiti wa Kijiji cha Soera, Wilaya ya Kondoa mkoani Dodoma, Shaban Maulid Simpi, amehukumiwa kifungo cha mwaka mmoja jela au kulipa faini ya Sh. Mil. 2.5 na kurejesha Sh. Mil. 1.46 alizofuja.

Februali mwaka huu mbele ya Hakimu, Lucas Jangandu, mahakama ya wilaya hiyo ilielezwa na Mwendesha Mashtaka wa TAKUKURU Mkoa wa Dodoma, Leonard Haule, kuwa fedha hizo zilitengwa kwa ujenzi wa Zahanati lakini Simpi, akazitumia kwa matumizi binafsi.

Awali, alikana kosa lakini kesi ilipokuja kwa ajili ya usikilizaji wa hoja za awali, akaomba akumbushwe shtaka lake na akakiri kosa.

Mshtakiwa huyo ameiomba mahakama impe muda wa kulipa faini, akapewa Siku 14 akishindwa atatumikia kifungo cha mwaka mmoja gerezani.